Burna Boy aandika historia Ufaransa

Burna Boy Aandika Historia Ufaransa

Moja ya story inayobamba katika mitandao huko ni ya msanii wa muziki kutokea nchini Nigeria Burna Boy ambaye ameandika historia ya kuujaza ukumbi wa Accor Arena mjini Paris Ufaransa.

Msanii huyo kutokea Afrika anaweka historia hiyo baada ya kuujaza ukumbi huo mara mbili sasa ambapo ameuza tiketi zote za tamasha lake la SpaceDrift kwenye ukumbi unaoingiza watu 20,000.

Awali Burna Boy aliwahi kuujaza ukumbi huo Novemba 10 mwaka jana na mwaka huu amefanikiwa kuujaza tena baada ya tiketi zote alizoziandaa kwaajili ya tamasha lake kuisha.

Tuambie unadhani ni msanii gani wa bongo anaweza kuujaza ukumbi huo au hakuna, tuwekee majibu yako katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii wa Instagram ambao ni @mwananchiscoop


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A writer, reporter, presenter and news anchor for Mwananchi Scoop. Her writings are based on Career and skills development every Monday and entertainment, every Friday on Mwananchi Scoop. Her famous segments on Mwananchi Scoop include SMARTPHONE and NIPE DILI.


Latest Post