Bumbuli aamishia majeshi NMB

Bumbuli aamishia majeshi NMB

Aliyekuwa msemaji wa ‘klabu’ ya Yanga Hassan Bumbuli aamishia majeshi Bank ya NMB akiwa kama Relationship Manager- sports and game.

Bumbuli tayari amefanya mabadiliko kwenye bio yake ya mtandao ya kijamii na kuandika Relationship Manager - Sports and Games #NMB Tanzania, #Former Media & Communications Officer #Yangasc.

Huku katika ukurasa wake wa #Instagram ame-share picha mpya yenye ujumbe usomekao,

“Ni heshima kubwa kwangu kujiunga na Bank bora Tanzania, ubora wa Bank ya NMB ni uliodhihirika katika kila nyanja, unanipa picha kwamba nimejiunga na ‘timu’ bora, imara nay a ushindi.

Ndugu zangu karibuni sana NMB Bank kwa huduma bora Zaidi za kifedha na zenye uhakika, saa 24 nchi nzima.”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags