Bruno akanusha kutimkia Saudi Arabia

Bruno akanusha kutimkia Saudi Arabia

Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa mchezaji #BrunoFernandes huenda akatimkia nchini #SaudiArabia mwisho wa msimu, staa huyo amekanusha na kusema anajisikia furaha kuendelea kuichezea Man United licha ya kipindi kigumu inachopitia timu hiyo.

Bruno ambaye ndiye nahodha wa sasa wa ‘timu’ hiyo amesema kwa sasa akili yake ameiwekeza kwenye kusaidia ‘timu’ yake ya  taifa ya #Ureno na Man United pekee.

"Kwenye timu ya taifa tunapata matokeo mazuri lakini kwa upande wa Man United hatujaanza vile ambavyo tulihitaji, siangalii tetesi na wala sizipi kipaumbele. Siku hizi ni rahisi sana kusambaza taarifa, lakini mimi sizijali naendelea kuweka umakini kwenye malengo yangu" amesema Brunio.

Hivi karibuni ziliibuka tetesi kwamba matajiri kutoka Saudia wamerudi tena na wameweka ‘ofa’ ya mshahara wa zaidi ya Pauni 100 milioni kwa mwaka ili kumpata mchezaji huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post