Bright muziki kwake kama kamari, Amkumbuka Ruge

Bright muziki kwake kama kamari, Amkumbuka Ruge

Na Aisha Charles

Miaka sita iliyopita alivuma sana na kibao cha ‘Umebalika’ alichofanya na Nandy ambacho kilikuwa na ujumbe mkubwa katika jamii na ndiyo wimbo uliovuma sana kila mtaa kutokana na ujumbe wake kuwagusa vijana na wazee huyu si mwingine ni Bright Music.

Ni miongoni mwa wasanii vijana usiweza kuwatilia shaka katika kufikisha ujumbe kwa hadhira na kuangalia video zake mbele ya mtu yeyote lakini alikaa kimya kwa muda mrefu takriban miaka sita bila tungo zake kutosikika masikioni.

Jarida hili la Mwananchi Scoop limefanya mahojiano na Bright ambapo amefunguka sababu ya ukimya wake.

Muziki ulivyo na faida kwake

Bright ameeleza kuwa pamoja na ukimya wake katika muziki haina maana kuwa ameuacha kwa sababu muziki ndiyo chanzo cha kumuwezesha katika biashara zake nyengine kama kilimo.

“Kwanza kabisa siwezi kuacha muziki kwa sababu ndiyo unaniwezesha katika biashara nyingine na kilimo kiujumla, maisha yangu yote mpaka uzee wangu nitafanya muziki ila kuhusiana na bishara pia nayo siwezi kuacha kwa sababu sisi watoto tuliozaliwa katika familia za hali ya kawaida lazima tujiongeze katika vitu vingi viweze kutupatia pesa ya kujikimu mahitaji yanayo tukabili”. Anasema

Anasema  muziki umemfanya aongeze juhudi ya kufanya mambo mengine na fursa mbalimbali katika jamii na bado anatilia nguvu zake katika muziki japo watu hawawezi kuona kwa urahisi ila ana kazi nyingi ambazo zinakuja zitakazoweza kumtambulisha zaidi.

Anaona muziki kama kamari

Hata hivyo Bright ameeleza chungu na tamu katika muziki amesema kuna muda muziki unakuwa kama kamali kwa sababu msanii anaweza kuwekeza pesa ili atoe wimbo na asipate kitu.

“Muziki ni kama kamari unaweza kuweka pesa kwa ajili ya wimbo na usipate kitu inakuwa imeenda na hiko kitu kinawakuta wanamuziki wengi  wa Bongo Fleva siyo mimi tu”. Anasema

Ruge alivyokuwa na malengo makubwa kwa Bright

Brihgt akuacha kumtaja marehemu Ruge Mutahaba katika mchango wake kwenye muziki ameeleza kuwa Ruge alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha anafanikiwa katika muziki na alikuwa na malengo makubwa ya kumuona msanii huyo akiwa mikononi mwake.

“Ruge ilikuwa kila interview ambazo alikuwa akifanya kuhusu wasanii anaowaangali kwa jicho la tatu mmoja wapo ni mimi alikuwa akinitaja sana na alikuwa na mipango mikubwa ya kunifikisha mbali kimuziki. Pia ni mtu ambaye alikuwa ana support kipaji changu tokea nilivyo toka Ifakara”. Anaeleza Bright

Sababu za kufanya wimbo na Nandy

Mwanamuziki huyu amefunguka pia sababu ya kufanya kolabo na Nandy katika wimbo wa ‘Umebadilika’ amedai kuwa wimbo huo alitakiwa afanye na mwanamuziki Ruby lakini manegment yake kwa kushirikiana na marehemu Ruge waliona inafaa kufanya na Nandy.

 

“Suala hilo lilikuwa nje ya uwezo wangu ni kweli Ruby alitakiwa awepo katika wimbo huo badala ya Nandy lakini management yangu ilikaa na marehemu Ruge ikaona inafaa kwa Nandy”. Anasema

Mahusiano yake na Belle 9

Asilimia kubwa ya watu walikuwa wanajua kuwa Bright ana undugu na Belle 9 lakini mwanamuziki huyu ameeleza kuwa hawana undugu wowote zaidi ya kuwa marafiki wa karibu tu. Kwa sababu Belle 9 ndiye aliyemtoa Bright kutoka Ifakara kuja Dar es salaam kwa ajili ya harakati zake za muziki.

“ Kiukweli hatuna undugu wowote japo tunatokea mkoa mmoja ila makabila tofauti na tunaurafiki wa karibu sana kwa sababu yeye pia ni mmoja kati watu walionishika mkono kuja Dar kufanya harakati zangu”. Anasema

Pia hakusita kuzungumza kuhusu Belle9 kuwa na mchango mkubwa katika kum-support kwenye kazi zake kama kaka yake na anamheshimu kwa sababu amemtoa mbali katika harakati za muziki.

Ndoto ya kufanya kazi na Best Naso

Kama ilivyo kawaida kwa kila mwanamuziki kuwa na ndoto ya kufanya kazi na msanii anayependa kazi zake basi kwa Bright kwake pia alikuwa na ndoto tangu anaanza muziki kufanya kazi na Best Naso na kwa bahati nzuri mwaka huu wametoa wimbo wa pamoja ‘Umasikini mbaya’ na mpaka sasa upo namba 14 on trending.

Hata hivyo anaamini kuwa wimbo huo utafika mbali kwa sababu unaujumbe ambao utawafikia kwa uzuri hadhira wa hali ya kwaida kutokana na maudhui ya wimbo.

 

“Ni ndoto ambayo nilikuwa naiota kila siku ya kuja kufanya kazi na Best Naso lakini Mungu mkubwa hatimaye mwaka 2023 mwishoni tulitengeneza wimbo kwa pamoja na tumeutoa wimbo huo tunaimani utafika mabali”. Anasema Bright
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags