BREAKING NEWS: Panya road 100 wakamatwa

BREAKING NEWS: Panya road 100 wakamatwa

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema zaidi ya wahalifu 100 wakiwemo vijana wanaofahamika kwa jina la Panya Road wamekamatwa ndani ya siku mbili wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kuvamia nyumba za watu, kupora mali na kuwa jeruhi.

“Wamekamatwa katika msako ulioanza September 14 ambapo doria zinafanyika katika mitaa yote ya Temeke,”amesema Jokate Mwegelo.

Aidha watuhumiwa hao wamekamatwa kutokana na  uvamizi uliofanywa September 12 na 13 katika kata za Mianzini, Chamazi na Kilungule.

Jokate amesema katika operesheni hiyo hawatawavumilia watendaji na viongozi wa mitaa wanaotoa ushirikiano kwa wahalifu au kuficha taarifa zao.

 “Hatutavumilia, kwahiyo wale wanaokaa vijiweni tutashughulika nao kama wachora ramani za uhalifu, tutawakamata wote sitakubali katika uongozi wangu Temeke iingie kwenye dosari ya vitendo vya uhalifu, ndio maana katika hili nasema tutakula sahani moja, hatuwezi kuwa tunapangiwa kazi na vijana wa hovyo,” amesema Jokate.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post