BOw WOw adaiwa kumtapeli mtoto wa miaka 10

BOw WOw adaiwa kumtapeli mtoto wa miaka 10

Rapper kutoka nchini Marekani Bow Wow ameshitakiwa kwa madai ya kutotimiza ahadi ya ‘kolabo’ licha ya kulipwa mamilioni ya pesa kwajili ya kufanya wimbo wa pamoja na binti wa miaka 10.

Kwa mujibu wa nyaraka za #Mahakama, msichana huyo akiwa na baba yake mzazi, walimlipa Bow Wow kiasi cha ($3,000) kupitia mtandao wa Cash App kwa ajili ya ‘kolabo’ lakini hakutimiza makubaliano hayo.

Baada ya makubaliano hayo kwenda tofauti mtoto huyo pamoja na baba yake, walifungua kesi ya madai na kutaka fidia ya zaidi ya milioni 30.

Kwa upande wake Bow Wow ameibuka kupitia ukurasa wake #Tweeter na kukanusha tuhuma hiyo kwa kudai kuwa , huwa haendeshi biashara zake kwenye Application na hasa hiyo ambayo imetajwa hapo, hajawahi kuitumia kabisa, hivyo huwenda wamepigwa na matapeli.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags