Boss mpya Man United kuanza na wawili

Boss mpya Man United kuanza na wawili

Inadaiwa kuwa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited kwa sasa ipo kwenye hatua nzuri ya kuwasainisha mikataba mipya ‘mastaa’ wao #VictorLindelof na Aaron Wan-Bissaka.

Sir Jim Ratcliffe ambaye amenunua hisa asilimia 25 hivi karibuni zinazomuwezesha kusimamia shughuli zote za mpira wa miguu amebariki suala hilo kwa asilimia mia wachezaji hao kupewa mikataba mipya.

Licha ya hayo Ratcliffe amepanga kujenga upya ‘timu’ hiyo kuanzia kwenye uongozi hadi ‘benchi’ la ufundi huku baadhi ya wachezaji kuuzwa dirisha dogo na mwisho wa msimu.

Man United imekuwa kwenye wakati mgumu kwa msimu huu ambapo inashika nafasi ya nane, baada ya kuchea mechi 18 na kukusanya pointi 28, pia ikiwa imetolewa kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na kwenye michuano ya Carabao.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags