Bosi ZIFF ataka wasanii kutunga filamu zinanzohusu jamii

Bosi ZIFF ataka wasanii kutunga filamu zinanzohusu jamii

Mwenyekiti wa Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Chande Omar amesema wanatarajia kuwasukuma wasanii kucheza na kutunga filamu zinazohusu changamoto za jamii na siyo mapenzi tu.

Omar ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 1, 2024 wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa 27 wa tamasha hilo.

"Tunatarajia katika tamasha linalokuja mwakani tufanye kazi karibu na Serikali hii kutokana na jambo moja tunakusudia kuwasukuma wasanii wa filamu kutengeneza filamu zinazohusu changamoto zilizopo kwenye jamii yetu hivi sasa.

Mfano suala la kuibiwa kwa watoto kudharilishwa watoto, ukosefu wa ajira ugumu wa maisha unaowakuta kina mama, hizi ni changamoto zilizopo katika jamii yetu na wasanii wa filamu wanakazi kubwa ya kuweza kuziwakilisha kwa jamii" amesema

Hata hivyo ameongeza ili kufanikisha hilo serikali inapaswa kuwaunga mkono ili wasanii waache kuigiza masuala ya mapenzi na badala yake wajikite kwenye changamoto za kijamii

"Lakini bila kupata ufadhili hawataweza kufanya kazi ambazo zinahitajika ili tuweze kupata uwezo sisi ZIFF lazima serikali yetu ituunge mkono sana.

Hatuwezi kuwaacha watengenezaji filamu waendelee kutengeneza filamu za mapenzi tu kuna mambo mengi ya kijamiii ambayo wanaweza kuyafanya yanamanufaa kwa jamii yetu,"amesema na kuongeza.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post