Boris Johnson ajiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uwaziri mkuu

Boris Johnson ajiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania uwaziri mkuu

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Boris Johnson, amesema hatawania nafasi ya kuwa mkuu wa chama cha Conservative nchini Uingereza.

Johnson amesema wabunge wengi walimpendekeza awanie nafasi hiyo kumrithi Liz Truss, lakini huu si muda muafaka kufanya hivyo. Hatua hiyo inakiacha kinyang’anyiro hicho wazi kwa waziri wa zamani wa fedha wa Uingereza Rishi Sunak.

Sunak anaungwa mkono na wabunge wengi wa Conservative kuwa Waziri Mkuu mpya. Sunak na Penny Mordaunt ndio wanasiasa wawili pekee wa chama hicho ambao wametangaza rasmi azma ya kuwania wadhifa huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags