Bora uvae viatu hivi au utembee peku

Bora uvae viatu hivi au utembee peku


Kampuni ya urembo kutoka Uhispania ya Balenciaga imezindua viatu viitwavyo ‘Zero’ ambacho ni mahususai kwa ajili ya kutumika katika msimu wa vuli mwaka 2025.

Viatu hivyo vimezinduliwa na Beini Quian, mkuu wa kitengo cha viatu Balenciaga kupitia Instagram yake vikiwa na kisigino na nafasi ya kidole gumba huku viatu hivyo vikipatikana kwa rangi nne tuu ambazo ni nyeusi, kahawia, nyeupe, na tan.



Hata hivyo, viatu hivyo kimepokelewa kwa maoni mseto mitandaoni, kutokana na baadhi ya watu kudai kuwa hakuna tofauti ya kuvaa viatu hivyo na kutembea peku.

Mdau mmoja aliandika, “Haiwezekani watu wanalipa Balenciaga maelfu ya dola ili kutembea kama wako peku.”

Kulingana na High Snobiety, hii si mara ya kwanza kwa Balenciaga kuunda viatu vya karibu na peku, kwani mwaka 2020 Quian aliwahi kuunda viatu kama hivyo ambavyo vilipewa jina la ‘Vibram’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags