Bongo hakuna wa kuniajiri, Lukamba

Bongo hakuna wa kuniajiri, Lukamba

Na Habiba Mohamed

Hellooow! Nyie nyie waswahili wanasema pata pesa tujue tabia yako yaani huo msemo haukukosewa kabisa maaana umetuoneshea sura halisi ya mpiga picha maarufu anaetambulika kwa jina la Lukamba.

Najua wengi wamemfahamu Lukamba kupitia msanii maarufu Diamond  alipomuajiri kuwa kumpiga picha wake binafsi basi bwana, Lukamba ameibua mjadala Kwenye mitandao ya kijamii baada ya video yake kusambaa mitandaoni akiwa anafanya mahojiano na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa kampuni  yake  ya kupiga picha ambayo aliipa jina la MAGIX MEDIA katika mahojiano hayo Lukamba alifunguka machache kuhusiana nayeye kuondoka wasafi na kuanzisha jambo lake

Lukamba alisema kuwa “Kuanzisha kitu chako haimaanishi kwamba unakuwa na ugomvi na Boss wako wa zamani au watu waliokutambulisha kwa mashabiki ni swala la ukuaji kibiashara zaidi" amesema Lukamba

Aidha aliendelea kwa kuongezea kwa kusema “sitaki kuajiriwa na msanii yoyote hapa bongo labda awe na levo za kumzidi Diamond  na sio kuniajiri , tunafanya kazi kila mtu anakuwa na maslahi yake"amesema

Haya haya wale wenzangu namimi swali la kujiuliza hapa kuna ulazima gani mtu kuacha kazi ambayo ilikuwa ikimpatia kipato kizuri na kuanzisha kitu kipya je nisahihi? Dondosha komenti yako hapo chini mwanangu sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags