Bondia Ryan Garcia afungiwa mwaka mmoja

Bondia Ryan Garcia afungiwa mwaka mmoja

Bondia wa ngumi za kuliwa kutoka Marekani Ryan Garcia amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya ngumi baada ya kuthibitika kutumia dawa iliyopigwa marufuku kabla na baada ya pambano.

Uamuzi huo umefanywa na Tume ya kupambana na dawa za kulevya Jimbo la New York baada ya Garcia kupimwa na kukutwa alitumia dawa ya ‘Ostarine’ kabla ya pambano lake la mwezi Aprili alilolichapa na bondia Devin Haney.

Licha ya kufungiwa mwaka mmoja pia atavuliwa ushindi wake katika pambano hilo lakini pia atatakiwa kurudisha pesa za ushindi alizolipwa kiasi cha dola 1.1 milioni huku akitakiwa kulipwa faini ya dola 10,000.

Hata hivyo ‘timu’ ya wanasheria wa Garcia ilikanusha madai hayo kwa kueleza kuwa bondia huyo hakuwahi kutumia dawa hiyo liyopigwa marufuku huku wakidai kuwa tuhuma hizo ni za kumchafua bondia huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags