Bondia Coleman anusurika na kifo kwenye ajali ya moto

Bondia Coleman anusurika na kifo kwenye ajali ya moto

Bingwa wa zamani wa UFC Mark Coleman (59) maarufu kama ‘The Hammer’ ameripotiwa kuwa katika hali mbaya hospitalini baada ya kuwaokoa wazazi wake katika ajali ya moto iliyotokea asubuhi ya Jana Jumanne huko Fremont, OH nchini Marekani.

Moto huo ulilipotiwa kutokea katika nyumba la ‘UFC Hall of Famer’ ambapo bondia huyo alikimbia ndani kuwaokoa wazazi wake Dan na Connie Foos Coleman, walipokuwa wamenasa kwenye chumba chao.

Aidha baada ya kufanikiwa kuokoa wazazi wake Mark alirudi kwa ajili ya kumuokoa mbwa wao lakini moshi ulimzidia na kudondoka chini, lakini alifanikiwa kuokolewa na kukimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa ndege.

Mark alijitokeza kwa mara ya kwanza katika eneo la michezo mchanganyiko ya kijeshi (MMA) mwaka wa 1996. Alinyakua mataji ya ubingwa wa uzito wa juu katika UFC mara 10 na UFC 11, aidha aliripoti kustaafu 2013.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags