Mshindi wa ndondi wa zamani nchini Urusi, Renat Agzamov, amegeukia kwenye utengenezaji keki zinazofanana na majumba ya hadithi za kale.
Kabla ya kuwa bondia, Renat akiwa na umri wa miaka saba alivutiwa na utengenezaji keki aliokuwa akifanya mama yake.
Licha ya kutumia sehemu kubwa ya ujana wake kwenye ndondi, Renat kwenye moja ya mahojiano yake alisema kwa sasa kupika hasa kutengeneza keki ndio kitu anachopenda zaidi, hivyo atabaki katika fani hiyo huku akipumzika katika ndondi na kudai hadi sasa tayari ametengeneza keki zaidi ya 3,000.
Kwa sasa Renat amejizolea umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa utengenezaji wake wa keki ajabu kwenye mitandao ya kijamii ana zaidi ya mashabiki milioni mbili
Leave a Reply