Mwigizaji kutoka Marekani Will Smith amedokeza ujio wa kurudishwa kwa filamu ya zamani ya ‘The Matrix’ akiweka wazi kuchukua nafasi ya Neo ambaye alikuwa ni muhusika mkuu.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Smith ameshare taarifa hiyo kupitia chapisho lake la zamani ambalo lilieleza jinsi alivyokataa kucheza filamu hiyo huku akiweka wazi kuwa kwa sasa yupo tayari kwa msimu mpya wa ‘The Matrix’.
Filamu hiyo imepangwa kuachiwa mfululizo wake mpya kwa miaka ya hivi karibuni ikiongozwa na Drew Goddard badala ya Wachowski ambaye aliiongoza filamu hiyo hapo awali.
‘The Matrix’ msimu wa kwanza iliachiwa rasmi Machi 1999 ikiwahusisha mastaa kama Keanu Reeves, Laurence Fishburne, Carrie-Anne Moss, Marcus Chong na wengineo.
Leave a Reply