Watu maarufu wanaomiliki  ndege

Watu maarufu wanaomiliki ndege

Umiliki wa ndege binafsi kwa watu maarufu ni moja ya kitu kinachoonekana kama mafanikio yao. Lakini pia hilo huusisha gharama za usafiri huo wa anga ambao wanamiliki. Wafahamu mastaa wanaomiliki ndege za gharama.

Drake, mkali huyo wa muziki wa hip-hop anamiliki ndege aina ya Boeing 767, yenye gharama ya dola 185 milioni sawa na Sh 489,540,000 bilioni.

Mwanamitindo na mfanyabiashara Kim Kardashian anamiliki ndege aina ya Gulfstream G650ER yenye thamani ya dola 150 milioni sawa na Sh396,900,000 bilioni

Tyler Perry ambaye ni mwigizaji maarufu kutoka Marekani anamiliki ndege aina ya Gulfstream III yenye gharama ya dola 125 milioni sawa na Sh330,750,000 bilioni

Mukesh Ambani ambaye ni bilionea maarufu kutoka India. Anamiliki ndege aina ya Boeing 737 Max 9 yenye gharama ya dola 118 milioni. Sawa Sh 312,408,000 bilioni.

Mjasiriamali, mhandisi, na mwekezaji maarufu kutoka Marekani Elon Musk anamiliki ndege aina ya Gulfstream G550 yenye gharama ya dola 78 milioni. Sawa na Sh206,268,000 bilioni.

Mjasiriamali maarufu kutoka Uingereza na mwanzilishi wa kampuni ya Virgin Group Richard Branson, anamiliki ndege aina ya Dassault Falcon 50EX yenye gharama ya dola 75 milioni, Sh198,450,000 bilioni

Mwanamitindo wa Marekani Kylie Jenner anamiliki Bombardier Global yenye gharama ya dola 73 milioni sawa na Sh193.4 bilioni






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags