Lody Music: Kushuka Kimuziki Hakunisumbui

Lody Music: Kushuka Kimuziki Hakunisumbui

Mwanamuziki wa Bongo Fleva aliyejizolea umaarufu kupitia wimbo wake ‘Kubali’, Lody Music ameiambia Mwananchi Scoop kuwa anaamini kupanda na kushuka ni sehemu ya maisha.

“Ukweli ni kwamba huwezi ukamzuia shabiki kuzungumza. Mara nyingi sijawahi kuwa na mawazo kwa watu wanavyosema nimepotea kwenye gemu, kwa sababu hamna mtu ambaye siku zote atakuwa juu, lazima upambane usiwe nyuma kabisa.

"Kushuka kwangu nachukulia kama hatua ya maisha, kwa sababu hata mwanzoni kabla ya wao kunijua nilikuwa huko na watu wakanijua lakini badaye mambo mengi yanatokea kuna muda chalenji za kimaisha zinatokea. Lakini mtu huwezi kujua unayopitia yeye anaongea tuu kwamba umepotea,” amesema Lody Music.

Lody Music ambaye amekuwa fundi wa kuwaandikia nyimbo mastaa, amesema shughuli hiyo imekuwa ikimsaidia sana kwani anafanya kama biashara.

“Uandishi ni biashara na sio kila mtu amebarikiwa kila muda awe anatoa ngoma na awe mwandishi. Kuna mtu amebarikiwa kujua kuimba lakini sio mwandishi, kuna mtu anajua kuandika lakini upande wa kuimba anakuwa havutii kabisa. Mimi niseme kwamba namshukuru Mungu kwamba naandika na Mungu anasaidia," amesema.

Ameongeza kuwa kwa kufanya hivyo haimaanishi kuwa anajisahau bali wasanii wanapenda uandishi wake hivyo anafanya nao biashara.

Utakumbuka Lody Music ameanza kusikika masikioni mwa watu mwaka 2021 kupitia wimbo wa ‘Kubali’, huku akitoa ngoma nyingine kama Kitambi, Hanipendi, Umenibadilisha, Nilizama, Kosa na sasa akitamba na ngoma ya Mahbuba aliyoaiachia mwezi mmoja uliopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags