Kampuni wa Swippitt ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vitu mbalimbali vya umeme wakati wa onesho la Ces 2025, imezindua kifaa maalumu cha umeme kiitwacho ‘Toaster’ ambacho kina uwezo wa kuchaji simu kwa sekunde mbili.
Kifaa hicho ambacho kimepokelewa kwa ukubwa kinauwezo wa kusaidi kuchaji simu yako na kujaa kufikia asilimia 100 ndani ya sekunde mbili tu ambapo teknolojia hii inafanya kazi kutoka asilimia 0 mpaka 100.
Kwa Sasa teknolojia hii inafanya kazi kwenye simu za Apple kuanzia Iphone 14, 15 na 16 huku ikiwa na mipango wa kuipanua zaidi teknolojia hiyo ili iweze kutumika kwenye simu za android kwa siku za mbeleni.
Programu hiyo pia inakuruhusu kuweka vigezo mbalimbali kama vile kuzuia kuchaji betri ya simu yako zaidi ya asilimia 80, kupanga muda maalumu wa kuchaji simu yako na mengineyo.
Leave a Reply