Diamond Aiteka Young Famous Africa Msimu Wa Tatu

Diamond Aiteka Young Famous Africa Msimu Wa Tatu

Mwanamuziki anyeupiga mwigi ndani na nje ya nchi Diamond ameendelea kuonesha ukumbwa wake kwenye reality show ya ‘Young, Famous & African’ baada ya video zake kuendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii huku akiwachanganya zaidi watu kwa kudai kuwa hana uhusiano na Zuchu.

Kupitia video baadhi zainazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii zimeibua mijadara mingi baada ya kuweka wazi kuwa Zuchu ni msanii wake tu na wala hana uhusianoa naye wowote.

“Unamaanisha Zuchu, sivyo ni msanii wangu sio mpenzi wangu, Ningekuwa mjinga kufanya hivyo. Wakati mwingine, wanawake wanahitaji kupewa maneno matamu huwezi kuwaambia ukweli. Ukifanya hivyo, hutawahi kuwafanya wakupende zaidi,” amesema Diamond

Aidha kutokana na kuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na kauli hiyo Simba kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi kuwa huo ni mchezo kama michezo mingine hivyo wasitumie video hizo kumuumiza Zuchu.

“Huo ni mchezo kama michezo mingine ‘Jua Kali’ na kadharika na character yangu humo ni hio mtu wa totoz, tutazame tuenjoy na tujivune kama watanzania tumeua na si kujaribu kukatakata vipande kwa lengo la kumuumiza Zyhura si vyema,” ameandika Zuchu

Licha ya kutoa kauli hiyo lakini wawili hao bado wameonesha uhasama mkubwa ambapo kwa sasa Diamond na Zuchu kila mmoja amefuta urafiki na mwenzake (unfollow) katika mtandao wa Instagram.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags