Huyu Ndiye Aaron Mwigizaji Anayedatisha Kina Dada

Huyu Ndiye Aaron Mwigizaji Anayedatisha Kina Dada

Kati ya picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuwadatisha baadhi ya kina dada, tangu mwishoni mwa 2024 hadi sasa 2025 ni za mwigizaji Aaron Stone Pierre ambaye ameigiza sauti ya Mufasa kwenye animation ya ‘Mufasa: The Lion King’.

Mfahamu zaidi. Nyota huyu alizaliwa Juni 7,1994 London nchini Uingereza asili yake ni Jamaica, alihitimu elimu yake ya juu katika Chuo cha London cha Muziki na Sanaa ya Kuigiza mwaka 2016.

Safari yake ya uigizaji ilianza mwaka 2018-19 baada ya kupewa jukumu la kuigiza kama Dev-Em katika tamthilia iliyohusisha maswala ya kisayansi iitwayo ‘Krypton’.

Tangu wakati huo ameendelea kuonesha kipaji chake katika filamu mbalimbali ikiwemo ‘The Underground Railroad (2021), Old (2021), Rebel Ridge (2024) huku akipata umaarufu zaidi baada ya kuigiza sauti katika ‘Mufasa: The Lion King’.

Februari 2022, Pierre alijiunga na waigizaji wa filamu ambayo itawahusisha mastaa kama Blade ambayo iko chini ya kampuni ya kutengeneza na kusambaza filamu ‘Maevel’ inayotarajiwa kutoka Novemba 7, 2025.

Aidha toka aanze kuwekeza muda wake katika filamu amewahi kushinda tuzo moja tu. Aliipata 2023 ambayo ni ‘Best Supporting Performance’ kupitia filamu ya ‘Brother’ akicheza kama Francis.

Mwigizaji huyo ameendelea kuonesha kipaji chake akiigiza katika filamu mbalimbali, huku akiwakosha baadhi ya kina dada mitandaoni wakiwemo mastaa Kutokana na mwonekano wake. Kati ya mastaa wanaovutiwa naye ni Tems wa Nigeria.

“Nina hisia za kimapenzi na Aaron Pierre ana sifa zote za aina ya mwanaume ninayemtaka,” Tems aliyasema hayo kwenye moja ya mahojiano yake nchini Marekani.
Mbali na maneno hayo ya Tems komenti nyingi kwenye mitandao ya kijamii ambazo huandikwa kwenye picha za mwigizaji huyo, huonesha wanawake wakimsifia na kuelezea hisia zao juu yake

“Eee Mungu tafadhali, huyu mwanaume anipende!!! 😩😭 LoL”

“Tafadhali Aaron chochote ufanyacho maishani, tafadhali usitangaze uhusiano wako, ndoa yako au ukweli kwamba huenda unamchumba kwenye mitandao hii ya kijamii πŸ™πŸΎπŸ™πŸΎπŸ™πŸΎ tafadhali naomba, nakusihi 😞 Hilo litakuja kuvunja moyo kwangu kwa namna kubwa zaidi katika maisha yangu yote πŸ’”πŸ’”πŸ’”πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­πŸ˜­,”

“Mwanaume wa ndoto yangu, jamani nampenda sana. Natamani na yeye anipende kama ninavyompenda”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags