Msanii wa muziki wa Injili, nchini Goodluck Gozbert amezua gumzo katika mitandao ya kijamii, baada ya kuchoma moto gari alilopewa na mmoja wa Manabii waliopo nchini huku akidai kuwa zawadi hiyo hakiwa sahihi kwake.
Kufuatia na video inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii msanii huyo amefunguka kuwa gari hiyo aliipokea kutoka kwa mtu ambaye sio sahihi jambo ambalo limepelekea kufanya uamuzi huo wa kuliteketeza kwa moto.
“Video inayoonekana hapo ni ya gari ambayo nilipokea kama zawadi toka kwa nabii mmoja hapa Tanzania mwezi Desemba mwaka 2021, ninayo mengi ya kuzungumzia lakini kwa sasa ningependa ijulikane ya kwamba chakula nilichoshiriki siku hiyo katika ibada hiyo na zawadi ya gari nililolipokea siku hiyo haikumpendeza Mungu.
Ninayemtumikia kwa sababu madhabahu hiyo haikuwa sahihi kwangu kushiriki na najua ya kwamba baada ya video hii kuwa imetoa itaibuka maoni tofauti tofauti ya watu pamoja na watumishi wengine wanaonipenda kwa wanaonichukia na yote ninayaheshimu, Mungu akinipa kibali cha kuzungumza kuhusu mengine basi nitazungumza kwa kadri ya neema niliyopewa kwa sasa nitasema haya machache na Mungu wa mbinguni awabariki sana,” amesema Goodluck
Hatua hiyo ya kuteketeza gari hilo imezua mijadala mikubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku wengine wakimsifu kwa ujasiri wake wa kulinda imani yake, wakati baadhi yao wakiona kama kitendo hicho hakikuwa na msingi.
Ikumbukwe kuwa miaka ya nyuma msanii huyo aliwahi kutamba na nyimbo kama Wacha Waone, Hauwezi Kushindana, Nimesamehe, Shukurani, Acha Waambiane huku wimbo wake wa mwisho kuuachi ukiwa ni Mbele Yako aliouachia miezi mitano iliyopita.
Leave a Reply