Chuchu Hancy Alia Na Aliyemzushia Kifo

Chuchu Hancy Alia Na Aliyemzushia Kifo

Mwigizaji Chuchu Hancy amekanusha taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai amefariki dunia.


Taarifa ya Chuchu kufariki ilichapishwa na mtumiaji wa mtandao wa TikTok aliyetambulika kwa jina la ‘Januari Mohamed’ akieleza kuwa amepokea taarifa kutoka kwa familia kuwa mwigizaji huyo amefariki dunia.

Kutokana na taarifa hiyo kusambaa na kuleta shinda kwa baadhi ya wanafamilia mwigizaji huyo amesema watu wanatakiwa kupuuza taarifa hiyo huku akiomba sheria kuchukua hatua kwa wanaowazushia watu kifo.

“Wewe Mungu mtu unaloniombea hili kuwa na huruma nimebaki peke yangu jamani kwenye tumbo la mamangu labda nikukumbushe miaka miwili iliyopita nimepoteza ndugu zangu wa tumbo moja mfululizo. Ukiwa unawatabiria au kuwaombea watu kifo au kuandika hakikisha unafatilia na familia yake.


“Haujawai ata kufikiria mamangu ambaye amebaki na mtoto mmoja atajisikiaje, atashtukaje mbaya zaidi niko nje ya Tanzania unajua familia yangu kiasi gani umeiumiza unajua watoto wa kakangu umewalizaje maana ni wakubwa na wanajitambua unajua watu umewatia safari kiasi gani siku zangu zikifika haitozuilika ila usijerudia hiki kitu aiseee,” ameeleza Chuchu


Aidha aliongezea kwuwa “Kama kuna sheria yoyote ya watu hawa ifanyie kazi. Kama ni akili yako Mungu anakuona ila akusamehe ila kama umetumwa waambie kwa uwezo wa Allah:(MUNGU) alienileta duniani basi yeye ndio ataniondoa siku aitakayo inshaallah,”


Chuchu sio msanii wa kwanza kuzushiwa kifo katika mitandao ya kijamii. Ambao taarifa zao zilizua taharuki kwa jamii akiwemo msanii wa nyimbo za injili Bony Mwaitege, Professor Jay na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags