Alichosema Ibraah kuhusu kufunga ndoa

Alichosema Ibraah kuhusu kufunga ndoa

Baada ya kusambaa kwa picha na video mbalimbali zikimwonyesha msanii wa Bongo Fleva, Ibraah akiwa Burudi alikokwenda kwa ajili ya kazi zake za sanaa na kuonana na familia ya mpenzi wake ni raia wa huko, inaelezwa akiwa huko amefunga ndoa.

Msanii huyo aliyeanza kutamba akiwa Konde Gang Music, alisema kwenda kwake huko mbali na kazi za muziki aliitwa na familia hiyo kabla ya kuzuka kwa picha hizo ingawa mwenyewe hajathibitisha kama ni kweli amefunga ndoa na dada huyo.

Tangu juzi usiku, katika mitandao ya kijamii zimesambaa picha na video hizo na watu kuanza kujiuliza kama ni kweli amefunga ndoa au ni kiki kwa ajili ya kazi zake au ni mpango wa kuachia video mpya kama ilibvyo kwa wasanii wengi nchini.

“Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuja Burundi na nimepokelewa vizuri sikufikiria kupolewa hivi, nimekuja kwa ajili ya mashabiki zangu na kuiona familia yangu,” alisema msanii huyo ambaye aliachana na lebo ya Konde Gang mapema mwezi uliopita.

Wakati huo huo, mkali huyo wa wimbo ‘Copy and Pest’ alisema yuko tayari kufanya kazi na nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kwani muziki ni biashara na hakuna kinachoshindikana.

Ibrah alisema hayo kwenye moja ya swali aliloulizwa na shabiki Burundi ikitokea kufanya kazi na Diamond atakuwa tayari.

“Hakuna kinachoshindikana kwenye kazi, ni kama wafanya biashara tu mnaelewana, kiasi fulani kama atakubali kwanini isiwe hivyo, ikitokea nitafanya kazi na Diamond,” alisema Ibraah.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags