193 wawekwa karantini ugonjwa wa Marburg

193 wawekwa karantini ugonjwa wa Marburg

Kufuatia ugonjwa hatari wa Marburg kutoka mkoani Kagera watu 193 wawekwa karantini kwaajili ya uchunguzi zaidi, Miongoni mwa watu hao ni watumishi wa afya 89 na wengine 104 kutoka kwenye jamii waliochangamana na wagonjwa na wote wanafuatiliwa maendeleo yao ya kiafya.

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu amesema zoezi linaendelea kuwafuatilia wote watakaobainika kuchangamana na wagonjwa wa Marburg

Watu watano wameripotiwa kufariki kutokana na Ugonjwa huo ulioibuka Machi 2023 katika Kata za Maruku na Kanyangereko, Wilayani Bukoba.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post