Binti wa Kinyalu akatimba ghetto na kudai hazioni siku zake…!

Binti wa Kinyalu akatimba ghetto na kudai hazioni siku zake…!

 

Basi binti alirudi kwao lakini kwa taarifa nilizokuja kuzipata baadaye kumbe usiku alianza kuvuja damu kwa wingi na tumbo kumuuma ikabidi wamuamshe dada yake ambapo kutokana na hali yake kuwa mbaya wakamkimbiza hospitali. 

Nilikuja kuambiwa kwamba hali ile ilisababisha kupoteza fahamu na baada ya madaktari kupambana sana walifanikiwa kuokoa Maisha yake lakini kila kitu kikawa hadharani kwamba alitoa Mimba.

Sasa zile habari zikavuja mtaani siku ya pili na ikawa inasemekana anasubiriwa atoke hospitali ili aulizwe ni nani alimpa mimba na aliyempeleka kuitoa na jina la hospitali. 

Mimi niliposikia hivyo nikajua ngondo igwa. 

Sasa ili kuepuka dhahama tukashauriana na jamaa niondoke pale kwa muda wakati yeye anasikilizia upepo hivyo nikamuaga kaka yangu kuwa naenda kwa kwa mama yangu mdogo kumsalimia kumbe nilikuwa nakimbia msala baada ya kuaga nikaondoka kimya kimya na kwenza Temeke kwa Sokota kwa huyo mama yangu mdogo. 

Lakini nilikwenda na Rafiki yangu ili ajue nilipo na ikitokea taarifa ambayo si nzuri aje kunijulisha. Hata hivyo sikumwambia mama mdogo kuhusu ile issue ya kumtia binti wa watu mimba na kuitoa. Nikasema tu nimekwenda kwake kubadilisha mazingira baada ya kukaa kwa kaka yangu kwa muda mrefu.

Basi bwana haikupita wiki moja binti akatoka hospitali na baada ya kubanwa akanitaja.

Kwa kuwa alikuwa hapajui kwa kaka yangu nilipokuwa ninaishi zaidi ya pale kwenye Gheto la mshikaji basi Polisi waliovaa kiraia wakafika pale kwa mshikaji wangu kunitafuta lakini jamaa sijui alishtuka walipofika kuniulizia akawaambia yeye ni mgeni pale hamjui huyo mtu wanayemtafuta. 

Wale Polisi wakaondoka ndipo jamaa akaja Temeka kunipa taarifa na kunishauri niondoke mjini niende kijijini kwa sababu amepata taarifa za chini chini kwamba shemeji wa binti ni shushushu kwa hiyo jela itanihusu. 

Baada ya taarifa ile nilianza kusikia maumivu ya tumbo la kuhara kwa sababu niliogopa sana. Ni kweli siku iliyofuata nikakamata basi la Born City pale Kisutu mpaka kijijini. Baada ya wiki moja nikiwa kijijini katika misele yangu nikapata taarifa kwamba kwetu kuna gari aina ya Landrover limekuja kutoka wilayani liko pale kwetu. Baada ya kupata zile taarifa nikaimbilia kwenye mashamba kujificha. 

Usiku nikarudi nyumbani kimachale nikaambiwa natafutwa na watu kutoka wilayani lakini hawakujitambulisha. 

Kwa kuwa nilikuwa ninajua kinachoendelea nikakata shauri kwenda kwa baba yangu mkubwa Kirinjiko kujificha na kule nikaingia kwenye kazi ya kusaidia kuchunga ng’ombe kazi ambayo sikuwahi kuifanya tangu kuzaliwa kwangu.

Ile kazi ya kuchunga sikuipenda kwa kweli kwa sababu ilikuwa na suluba kweli kweli maana kuna jua kali na ile hali ya kushinda porini ilinikera sana kwa kweli. 

Hebu fikiria kijana Bitozi wa Jijini Dar anayejua kuoga kupiga pamba zilizopigwa pasi kwa umahiri na raba mtoni leo unamwambia ashike fimbo akachunge ng’ombe, yaani mpaka nikakumbuka kitabu cha mwandishi mmoja kule Kenya kinachoitwa Is it possible? Kilichotungwa na Henry R. ole Kulet.

Life is not fair kwa kweli.

Basi niliishi kwa baba yangu mkubwa kwa miezi miwili na mwaka mpya wa 1993 ukanikuta huko lakini kutokana na mazingira kuwa magumu nikarudi kijijini  nikijisemea liwalo na liwe.

Kwa bahati nzuri nikiwa kijijini akaja kaka yangu mwingine ambaye alikuwa ni meneja wa benki mkoani Morogoro. Alishangaa kunikuta kijijini. Aliponidadisi kama ninasoma nikamweleleza kila kitu kuhusu kumaliza chuo cha ufundi na ile changamoto ya kumtiaq binti wa shule Mimba na kukimbilia kijijini kujificha…. 

Basi kwa kuwa kaka alikuja kijijini likizo wakashauriana na baba anichukue nihamie Morogoro akanitafutie kazi kwenye kiwanda cha Tumbaku au kwenye Karakana ya Railways. 

Ni kweli, nilihamia Morogoro na kuanza maisha upya lakini nikiwa nimejifunza kwamba kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike ni sawa na kubisha hodi jela, muda wowote utafunguliwa. 

mwisho

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Mzee Mtambuzi

A freelance Journalist and also teaching self-empowerment, positive thinking as a means of creating the life you desire including spirituality. He is writing in Mwananchi Scoop every Wednesday Visa na Mikasa.


Latest Post