Binti mwenye nywele nyingi zaidi duniani

Binti mwenye nywele nyingi zaidi duniani

Dunia ina mengi ya kujifunza kila kukicha , kuna wakati matukio yanatokea kwa sababu jamii haina elimu ya kutosha kuhusiana na mambo fulani, ni vyema kwenye jamii kwanzia ngazi za familia kujazana elimu dhidi ya upendo bila kujali, kasoro zilizopo miongoni mwa wanafamilia.

Mfahamu Supatra Sasuphan kutoka Thailand, binti nywele nyingi zaidi #Duniani, ambaye licha ya kuwa na nywele mwili mzima lakini familia na jamii kwa ujumla, haikusita kuonesha upendo kwake hadi kupelekea binti huyo kuingia kwenye Kitabu cha Rekodi Za Dunia za Guinness.

Supatra alizaliwa mwaka 1999 akiwa na nywele nyingi zilizofunika kila sehemu ya mwili wake, jambo lililopelekea wazazi na jamii nzima kuhamaki aina ya mtoto ambaye amezaliwa , lakini utofauti wake bado haukuwa changamoto, kwani aliendelea kupata upendo kutoka kwa watu wake wa karibu ikiwemo wazazi wake.



Wingi wa nywele wa Supatra unaelezwa kuwa ni ugonjwa wa mabadiliko ya DNA unaopelekea nywele kukua kwa kasi kila sehemu ya mwili isipokuwa kwenye viganja tu. Kutokana na nywele zake kukua kwa haraka alipofika umri wa miaka 10 lianza kunyoa uso wake ili kuzipunguza na ndivyo anavyofanya hadi sasa lakini bado haisaidii kitu.

Ndipo mwaka 2010 #Dunia kwa ujumla ikamfahamu baada ya kutambulishwa na #Guinness kama binti mwenye nywele nyingi zaidi Duniani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags