Billnass: Bado kidogo ndoa isifungwe

Billnass: Bado kidogo ndoa isifungwe

Na Habiba Mohammed

Ebwana niaje mtu wangu wa nguvu. Ni muda wa mastori na kawaida lengo letu ni kuzitafuta na kukuletea habari moto moto kuhusu mastaa wako ili uweze kujifunza na kuburudika. Kila jambo la kheri halikosi vikwazo ni maneno ya waswahili, basi bhana mkali wa bongo fleva 'Mafioso' ama Billnass afunguka kusema bado kidogo ndoa isifungwe.

Msanii huyo katika mahojiano katika chombo kikubwa cha habari  amefunga juu ya vikwazo walivyokutana navyo katika maandalizi ya harusi yake.

“Mambo yalitokea mengi kabla ya ndoa ila ambalo sitasahau nilichelewa kupata nguo zangu kwa wakati na ndoa yetu ilipangwa kufungwa asubuhi, pia kwa upande wa mke wangu Nandy alipata changamoto kwa baadhi ya wasimamizi wake kutaka kujitoa,” amesema msanii huyo.

 Pia aliongezea kusema, “kanisani tulipata changamoto licha ya kujaza fomu zote lakini siku ya ndoa kulitokea mvutano ilihali taratibu zote tulikamilisha ili nibidi nitulize akili na kushirikiana na watu wa karibu ili ndoa iweze kufungwa.’’ 

“Wakati huo huo nikawa na changamoto ya usafiri maana gari zote nilizolipia hazikuweza kufika ikabidi kamati yangu iweze kunisaidia kutatua hiyo changamoto,” amesema Billnass.

Alooooh! Sio mchezo mambo yalikuwa mengi kwahiyo hata lile jicho la mke wa Nenga lilikuwa hasira aisee. Shusha comment yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags