Imezoeleka kuwa watu wengi wakipata pesa hubadili mienendo yao, na aina ya maisha waliyokuwa wakiishi mwanzo, lakini hii ni tofauti kwa Jeff Bezos, mwanzilishi wa kampuni ya Amazon, kwani bado anafanya kazi katika kiti na meza ile ile aliyokuwa akitumia wakati anaanzisha kampuni hiyo.
Licha ya kutajwa kuwa miongoni mwa matajiri duniani , lakini Jeff anatumia kiti na meza ya tangu mwaka 1994, kama ishara ya utamaduni wa Amazon, yeye si wa kwanza kuitumia pia vitu hivyo viliwahi kutumiwa na wafanyakazi wa awali wa Amazon, wakionesha kujitolea kwa kutumia pesa kwa mambo ambayo yananufaisha wateja badala ya gharama zisizo za lazima.
Licha ya kuwa kampuni hiyo ni miongoni mwa zinazofanya vizuri duniani kote, lakini imekuwa ikitumia kiti na meza za aina hiyo kwa lengo la kuendeleza utamaduni kama ukumbusho wa mwanzo wa kampuni na maadili yake ya kudumu.
Amazon ni kampuni ya teknolojia ya kimataifa ya Kimarekani ilianzishwa mwaka 1994. Inachukuliwa kuwa moja kati ya kampuni kubwa tano za teknolojia Amerika nyingine nne nizikiwa ni Alphabet, Apple, Meta, na Microsoft.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply