Bifu la Shilole na Alikiba lafikia patamu

Bifu la Shilole na Alikiba lafikia patamu

Ee bwana mtu wangu wa nguvu huko mitandaoni kuanzia jana hadi leo moja ya story inayobamba ni kati ya wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya Zuwena maarufu kama Shilole na Alikiba kurushiana maneo mazito.

Akihojiwa katika moja ya kituo cha televisheni, Alikiba alisikia akisema hakumualika Shilole katika party yake ya uzinduzi wa albamu jambo ambalo lilimuibua Shilole na kutokwa na povu katika ukurasa wake wa Instagram.

Kupitia Insta yake Shilole aliandika kuwa:- “Hapana jamani, kila siku nakosewa nikitaka kuongea washauri wangu wanasema nikae kimya. hili nimekosewa sana na siwezi kukaa kimya sasa mnanionea. @officialikiba nakushukuru sana leo umeuthibitishia ulimwengu mambo yafuatayo :

“Huna kiburi cha kishamba, unavimba na kupandisha mabega katika namna isiyostahili. Huna utu ambao watu wako wanakupamba kwamba uko nao. Sawa mimi na wewe hatuna mazoea (Hilo ni kweli kabisa), lakini mimi na wewe tupo katika field moja.

“Ningeweza kuja kwenye shughuli yako kuonesha upendo tu hata kama sijaalikwa, ungekuwa na utu, haikuwa na haja kwenda redio na kusema “SIJAMULIKA” : ili mimi nionekane nilivamia tu shughuli tu?. Shame on you Ali. (ila kwa tabia zile za kwenda Marekani kuomba dada zako naniliu hushangazi)

“Umethibitisha kwamba wewe hauko ‘organized’. Kwa sababu, utasema nilipostiwa kwenye page yako na kutafutwa na watu wako wakati hawajakutaarifu. Kwa hiyo kwa ukubwa tunaotangaziwa unao Bwana Ali, unataka kusema hujui hata kilichopostiwa kwenye page yako rasmi katika siku yako muhimu? Kwa hiyo hata Nasibu uliyeshindana naye miaka mingi akakugaragaza angeweza kualikwa bila wewe kujua? (Nasibu humuwezi tusikudanganye). Wewe ndo msanii wetu wa kimataifa? Sijapenda,”

Hayo ni baadhi ya maneno aliyoyaandika Shilole jambo ambalo limefikiriwa kuwa wwaili hao sasa wameingia katika bifu nzito sana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags