Biden aweka saini sheria itakayoweza kuindoa tiktok Marekani

Biden aweka saini sheria itakayoweza kuindoa tiktok Marekani

Rais wa Marekani Joe Biden ametia saini muswada wa sheria ambao endapo utakiukwa mtandao wa TikTok utapigwa marufuku kutumika nchini humo.

Baraza la wawakilishi la Bunge la Marekani lilipitisha muswada huo Jumamosi, huku Baraza la Senet likiidhinisha muswada huo siku ya Jumanne usiku.

Sheria hiyo mpya inampatia miezi 9 mmiliki wa mtandao huo kutoka nchini China Shou Zi Chew kuuza sehemu ya uthibiti wake la sivyo TikTok itapigwa marufuku nchini humo.

Hata hivyo kwa upande wa Shou ameonesha kupinga muswada huo akidai kuwa hatua hiyo ni mpango wa wanasiasa nchini humo kuwaminya raia wake ambao wamekuwa wakitumia mtandao huo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags