Biden amepongeza uteuzi wa Rais wa Benki ya dunia

Biden amepongeza uteuzi wa Rais wa Benki ya dunia

Rais wa Marekani Joe Biden amempongeza kiongozi mpya wa benki ya dunia Biden Ajay Banga siku ya jumatano kuwa ni kiongozi mwanamageuzi

Rais ambaye atajumuisha mabadiliko ya hali ya hewa kwenye orodha ya changamoto ambazo taasisi hiyo inakabiliwa nazo katika kazi zake kwenye mataifa yanayo endelea.

“Ajay Banga, atakuwa kiongozi atakayeleta mabadiliko, kuleta utaalamu, na ubunifu katika nafasi yake kama rais wa benki ya dunia,” alisema Rais Biden katika taarifa yake.

Sambamba na hayo aliyekuwa Rais wa benki ya dunia David Malpass, alijiuzulu mwezi Febuari baada ya kutoa kauli zilizo ashiria kupuuzia masuala ya mabadiliko ya hali hewa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags