Bibi wa miaka 84 aliyechagua rangi ya kijani kuendesha maisha yake

Bibi wa miaka 84 aliyechagua rangi ya kijani kuendesha maisha yake

Imekuwa jambo la kawaida kwa wanawake na mabinti kuvutiwa na rangi ya ‘Pinki’ huku baadhi yao wakipendelea kuwa na vitu vya rangi hiyo kwa madai ya kuwa inawapa muonekano mzuri.

Katika jamii ya sasa ni ngumu sana kumkuta mtu amevaa rangi moja kuanzia juu hadi chini , watu wengi hupenda kuchanganya rangi, lakini jambo hilo ni tofauti kwa Elizabeth Eaton Rosenthal, (82) maarufu kama Green Lady, kutoka nchini Marekani.

Zaidi ya miaka 20 sasa Green Lady amekuwa akivaa nguo na vitu vya  rangi ya kijani kuanzia juu mpaka chini huku akidai sababu iliyomsukuma kuwa na muonekano wa rangi hiyo ni kuwafanya watu watabasamu.

Siyo kuvaa tu bali hata vitu anavyomiliki vina rangi ya kijani, imebidi  mume wake naye akitoka kwenda sehemu lazima avalie kitu chenye  rangi hiyo, kutokana na muonekano wake watu wengi wamekuwa wakimiminika nyumbani kwake kwa ajili ya kupiga naye picha kama kivutio.

Green Lady amepata wafuasi wengi kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya kuwa na muonekano wa tofauti na wengine. huku familia moja kutoka nchini humo kufata nyayo za bibi huyo kwa kumvalisha mtoto wao nguo za rangi hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags