Bibi wa miaka 78 ashtakiwa kwa wizi banki

Bibi wa miaka 78 ashtakiwa kwa wizi banki

Na Asha Charles

Hahahah! Make hapa kwanza ncheke, ama kweli hali ngumu basi bwana unaambiwa bibi aliejuliakana kwa jina la Bonnie Gooch mwenye umri wa miaka 78, ameshtakiwa kwa kosa la wizi kwa kuiba katika taasisi za benki nchini Marekani pamoja na uzee wake alionao.

Bibi huyo amewahi kukutwa na hatia mara mbili zamani kwa wizi wa benki moja ya matukio hayo ya wizi yalitokea huko California nchini Marekani mnamo 1977 na nyingine mnamo mwaka 2020.

Hivi karibuni  bibi huyo aliingia katika benki ya Goppert na kudaiwa kukabidhi barua kwa mhudumu akidai maelfu ya pesa tasilimu na kuwa laghai wahudumu wa hapo kwa hali ya kawaida bibi kama huyo nirahisi kumuamini.

Polisi katika jimbo la Missouri Marekani walipigwa na butwaa baada ya kugundua mwizi aliyepora maelfu ya dola katika benki hiyo alikuwa ni bibi kizee.

Mkuu wa polisi wa pleasant hill, Tommy Wright aliambia gazeti la Kansas city star kuwa “hatukuwa na uhakika hapo awali kwamba tulikua tumemkamata mtu sahihi” alisema mkuu wa polisi

Mpaka sasa bibi huyo yupo gerezani akitaka dhamana dhidi ya mashtaka hayo huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi zaidi.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags