Bibi harusi mtarajiwa aliyefariki ajalini kuzikwa leo

Bibi harusi mtarajiwa aliyefariki ajalini kuzikwa leo

Amani Mollel, ambaye alikuwa ni bwana harusi mtarajiwa wa Rehema Chao, (wa kwanza kulia), akiwa amebeba msalaba wa mpendwa wake aliyefariki ajalini wailayani Mwanga, Mkoani Kilimanjaro, akitokea kwenye ‘send-off’ yake iliyofanyika Novemba 24, mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake ambayo ilikuwa ifanyike leo, Desemba 2, katika Usharika wa Oldonyosambo, mkoani Arusha.

Bibi harusi huyo alipata ajali Novemba 28, mwaka huu katika eneo la Kichwa cha Ng'ombe, wilayani Mwanga baada ya gari alilokuwa akiendesha aina ya Raum kugongana na lori wakati akikwepa shimo.

Katika ajali hiyo alifariki mama yake mzazi, Agnes Chao (75) na msichana wa kazi, Irene Shija (15) mkazi wa Geita. Picha na Janeth Joseph.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags