Bibi harusi afyatua risasi kwenye harusi yake na kukimbia

Bibi harusi afyatua risasi kwenye harusi yake na kukimbia

Hahahah! Ama kweli ukistaajabu ya mussa utayaona ya firauni, sasa hapa ndo nayaona basi bwana polisi kutoka nchini India katika jimbo la Uttar Pradesh wanamsaka mwanamke aliyefyatua risasi kwenye harusi yake na kukimbia.

Video ambayo imezua taharuki kubwa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha mwanamke huyo akifyatua risasi nne hewani akiwa amekaa karibu na mumewe.

Polisi wa eneo hilo walisema wameandikisha kesi dhidi ya mwanamke huyo ambaye ametoweka tangu tukio hilo kutokea.

Milio ya risasi wakati wa harusi ni jambo la kawaida katika baadhi ya majimbo ya kaskazini mwa India na mara nyingi husababisha majeraha na hata vifo .

Kulingana na sheria za India, mtu yeyote anayetumia bunduki kwa kutowajibika au kwa uzembe au kusherehekea na kuwaweka wengine hatarini anaweza kufungwa jela au faini au vyote kwa pamoja. 

Aidha polisi waliambia jarida la Times of India kuwa mwanamke huyo "ametoroka" kwa sababu aliogopa kukamatwa.  

Duuuuuh! Sijui tuseme ni furaha ilizidi ama aliamua tuu, embu dondosha komenti yako utueleze mtazamo wako wewe mdau wetu kuhusiana na hili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags