Biashara zenye mtaji usiozidi Tshs 50k

Biashara zenye mtaji usiozidi Tshs 50k

Mambo vipi kijana mwenzangu? leo kwenye nipe dili nakusogezea biashara zenye mtaji mdogo usiozidi Tshs 50,000 ambazo unaweza kuzifanya na zenye faida kubwa.

Amini kwamba  zipo biashara ambazo unaweza kuanza na mtaji mdogo na zikakuletea faida kubwa ukiifanya kwa ubora wa hali ya juu na bidii ipo siku utatoboa tu mtu wangu.

  • Kufundisha

Kijana jiamini hakika unaweza kufundisha chochote kile unachokijua ikiwa kuna watu wanahitaji kujifunza hata usiende mbali hapo hapo ulipo jitathmini kwa kujiuliza machache tu je watu wanahitaji kujifunza nini? 

Tayari hilo ni dili watafute hao watu kisha onyesha uwezo wako bwana taaluma sio lazima hesabu, au sayansi chochote unachokifahamu vizuri basi kitumie.

  • Kupika kwa Oda

Enhee hapa sasa changamkia fursa kama wewe ni mpishi mzuri au una mtu anayejua kupika, basi jitangaze kama unapokea oda za mapishi Fulani, mfano unaweza kupika biriyani vizuri na sasa chakula hicho ndo habari ya mjini.

 

Unachoweza kufanya ni kwenda maofisi ya karibu yako nakuanza kwenda  kwenye maofisi mbalimbali na kuwataarifu kuwa wakutatufe wanapohitaji chakula .

 

Usisahahau kuacha mawaziliano kwani ndiyo mbinu yako hiyo yakupata wateja kwa urahisi.

 

  • Kupiga picha

Hii nayo imekaa poa sana mtu wangu kama ukiifanya vizuri itakutoa kuwepo kwa mitandao ya kijamii kama vile Instagram, facebook watumiaji wa mitandao hiyo wanahitaji picha nzuri ili wajidai nazo huko.

 

Hapo ndipo kwakukazania wewe na kusimamia mchongo huo, hakika kazi hii ni kazi kama nyengine ili uwe bora zaidi kwanza kuwa mbunifu yaani lazima uwe tofauti na wengine, usiogope vifaa unaweza kukodi au kuazima kwa washkaji na ukapiga kazi vilevile.

 

  • Kupamba maharusi

Hili ni bonge la dili mtu wangu kwani hakuna ambaye hapendi kupendeza siku ya harusi yake, ili upendeze harusini wanandoa lazima wapambwe.

 

 Jitahidi kutafuta mtu mwenye ujuzi huu na kumuomba uwe unapamba nawewe ikiwezekana usitake malipo ili uweze kupata ujuzi mwingi zaidi ukitoka hapo tayari umefanikisha unaendelea na ujuzi wako.

 

  • Kununua na kuuza

Biashara hii nayo itakutoa ukiizingatia ili uwe mjasiriamali mzuri lazima utambue thamani ya vitu kabla wengine hawajaviona

 

Hivyo, tafuta bidhaa ambazo zinauzwa kwa bei ya chini, zinunue na utafute soko ambalo hizo bidhaa zinauzwa kwa bei ya juu uende ukaziuze huko.

 

Unaweza kununua bidhaa Dar es salaam ukazisafirisha mikoani bila usumbufu na ukapata pesa nzuri tu.

 

Kijana mwenzangu fahamu kuwa hakuna biashara ndogo, ili ufanikiwe kwenye biashara yako hakikisha unakuwa na uvumilivu, kutokukata tamaa, jifunze kwa wengine ongeza juhudi utatoboa tu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags