Biashara za mtandaoni zinazolipa zaidi

Biashara za mtandaoni zinazolipa zaidi

Hellow! Niaje watu wangu wa nguvu wa Mwananchi Scoop, I hope mko pouwa kabisa, sasa leo katika biashara tuko na mada ambayo najua wengi mshazoea blabla mnazo sikia mitaani sasa leo tumekusogezea ile yenyewe.

Kwanza kabla hujaamua kuanza kufanya biashara ya mtandaoni unatakiwa kufuatilia biashara unayotaka kuifanya uuzaji wake, faida hasara na wenzako waliotangulia katika biashara hiyo wanaiendeshaje.

Najua mnajua kuna biashara nyingi za kuzifanya mitandaoni lakini si kama mnavyo elewa kuna baadhi ya biashara hazitakiwi kabisha kufanywa online yaani mtandaoni ila tunaforce tuu.

Kuna orodha ndefu ya biashara za mtandaoni zenye faida barani Afrika. Baadhi zao ni…

  • Bidhaa za Mapambo ya Ulimbwende na urembo

Katika ulimwengu wa kisasa, kila mtu anataka kuonekana vizuri na aingiane sawasawa na mitindo inayovuma. Unaweza kupata pesa kupitia dhana hii kwa kuuza bidhaa kama vile nguo, viatu, mapambo ya vito, bidhaa nywele, marashi, na mikoba. Kulingana na mtaji wako na wateja walengwa, unaweza kupata bidhaa mpya kabisa au hata zilizotumika kiasi.

Cha  muhimu cha kufanya hapa niwewe kuendana na trends za mavazi, kama kipindi hichi watu hupendelea sana kushona nguo za vitambaa, may be kuvaa mabaibui, unatakiwa kuendana na upepo wa biashara.

  • Bidhaa za Uboreshaji Nyumbani

Watu wengi wana hamu ya kupata bidhaa ambazo zinaweza kubadilisha nyumba zao ziwe makazi bora zaidi, mfano kapeti za chini, shuka and duvert, picture, saa, walpape za ukutani nk.

Siku hizi watu wengi wako hivi ni bora asile chakula kizuri asinywee lakini chumbani kwake ukiingia lazima ushikwe na butwaa, kama nilivyosema hapo awali inabidi uendane na upepo wa biashara sasahivi watu wengi wanapenda kupendezesha makazi yao kuliko kitu chochote kile.

  • Bidhaa za Watoto

Wazazi wa kisasa wako tayari kugharamika Zaidi ili kuhakikisha kwamba watoto wao wana maisha mazuri. Vifaa bandia vya kuchezea, nguo za kimitindo pamoja na vifaa vinginevyo vya kuwalea watoto vimekuwa sasa mahitaji ya kimsingi, na wala si vya kifahari. Kwa hivyo, mtu anaweza kuwa na biashara yenye faida kwa kuziuza kupitia mitandao ya kijamii.

Hii biashara inalipa sana kama tuu ukiwa serious nayo, zile zama za kumvesha mtoto nguo mpka akue nayo zimeshapitwa na wakati siku hizi watu wanaenda na muda so jaribu utakuja kunishukuru badae hili ni bonge la biashara hutakuja kujutia pesa yako ya mtaji kamwee.

 

  • Huduma za Ushauri wa Kibiashara

Hii ni mojawapo ya sekta kubwa ya huduma za kitaalamu duniani. Kuna kazi nyingi za ushauri ambazo mtu anaweza kuzishiriki kupitia teknolojia.

Hizi ni pamoja na mahusiano ya umma (public relations), uongozi, mauzo (marketing), kazi, na ushauri wa kimawasiliano (communications consultancy). Hii ni biashara ya kufanya hata ukiwa nyumbani.

  • Kutoa huduma za Matukio na Sherehe

Biashara hii inakuwa hivi unanunua vitu ambavyo ni vyamuhumu kabisa katika shughuli mfano viti, sufuria, sahani, maturubai, majaba ya kuwekea maji na vitu vinavyohusiana na sherehe, unakuwa unavikukodisha katika sherehe mbalimbali.

Huduma kama hizi zimepata sana uhitaji katika harusi, mazishi, sherehe za kumbukumbu za kuzaliwa, mikutano ya kampuni, na hata mikusanyiko ya kawaida ya familia so wewe ukiamua kufanya hivyo basi utakuwa umeupiga mwingi sana maana pesa yako ya mtaji itarudi kwa muda mfupi tuu.

  • Huduma ya Vyakula

Ukuaji wa miji na kuongezeka kwa idadi ya wataalamu ni baadhi ya mambo ambayo yamechangia kuongezeka kwa mahitaji ya maduka ya vyakula mtandaoni.

Idadi kubwa ya waajiriwa katika miji ya Afrika iliyoendelea na hata inayoendelea hukosa muda wa kununua vyakula. Badala yake, unaweza kutoa huduma hiyo kwa kuwafanyia watu delivery, mfano kama Mudi mabiriani huwa anapika chakula na kuwapelekea watu popote watakapo.

Sio lazima uanzishe biashara ya kuuza chakula, unaweza kuuza hata kuku wabichi, samaki, dagaa, mboga za majani na ukafanya delivery   ukapata na wateja changamka muda ni wako sasa.

Oooooh! I hope tuko pamoja watu wangu wa nguvu acha kuwa beki tatu jishughulishe wewe, acha kutumia bando lako kwa kuangalia umbea wa mitandaoni na kuwasema vibaya wasanii, hilo hilo bando la jero tumia kutangaza biashara yako ndugu yangu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags