Biashara ya madera na vijora inavyo shamiri mjini

Na Aisha Lungato

Hapo zamani kanga ilikuwa sare ya msiba au sherehe, lakini hivi sasa vazi la madera na vijora limechukua nafasi ya khanga.

Sio tu kwa ajili ya sare bali mavazi haya yamejipatia umaarufu kuanzia miaka ya elfu mbili na kupendwa na wanawake wengi, hususani waishio maeneo ya pwani na mijini. 

Mwananchi Scoop tulifanya mahojiano na mwanadada Irene Bernard ambaye ni mkazi wa Tabata ameeleza kwamba wanawake hupendelea kuvaa nguo hizo kwasababu ni nguo ambazo huwafanya kuwa na amani kwa kutowabana na kutonyesha maumbile yao.

“Hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam pia huchangia kutokana na joto, hivyo wanawake hawapendelei kuvaa nguo zilizo wabana badala yake huangukia katika nguo hizo dera, vijora, baibui,” alisema Irene.

Irene anasema kwa upande wake anapenda kuvaa kijora kwa sababu kinamfanya awe huru hata akiwa ameshinda nyumbani. Anasema hawezi kuvaa kanga au gauni halafu akashinda nyumbani. Akamalizia kwa kusema anaamini mavazi hayo ni ya mtoko peke yake.

Wakati Irene anatueleza hayo, Mariam Ismail mkazi wa Msasani anasema unafuu wa vazi hilo ndio sababu huwafanya wanawake wengi kulipenda, aliongeza kwamba mtu akivaa kijora sio rahisi kwa watu wengine kuyaona maumbile yake ya ndani kwani ni vazi ambalo linawasitiri vizuri.

“Vazi hilo linatusitiri sehemu zote za mwili jambo ambalo pia ni zuri kutokana na kwamba ni vazi lililozingatia maadili mema,” alisema Mariam.
 
Naye Prisca Tumaini kutoka Kibaha, anasema vazi hilo kwa upande wake  hulitumia wakati wa shughuli akimaanisha wakati wa sherehe, kama harusi, ngoma lakini si kama vazi rasmi la kutokea.

“Mimi siwezi kuvaa kijora naona kama vazi ambalo linavaliwa sana na watu wengi, kwa upande wangu naona kama halijakaa kimaadili,” alisema 

Prisca anasema mtu huwezi kuvaa dera au kijora ukatoka kwenda kwenye sehemu za heshima, akitolea mfano mtu kama mwalimu hawezi kwenda darasani amevaa kijora au dera halafu akafundisha.  

Kwa upande wa wafanyabiashara wenyewe wanafurahia mavazi hayo kwa sababu yanauzika sana, tofauti na vazi aina ya kanga huku wakisema wasichana ndio wanunuaji wakubwa. 

Kulthoum Soud mfanyabiashara anayejihusisha na uuzaji wa aina hizo za nguo, ambaye anaduka maeneo ya Airport jijini hapa, anasema bei ya vijora huwa anauza kuanzia Tsh 6000 mpaka Tsh 35000 huku wanawake wa kuanzia umri miaka 19 mpaka 45 wakiwa ndio wanunuzi wengi.

“Wateja wangu wengi kwa asilimia zaidi ya 80 huwa ni wanawake, kwani wengi wao hupendelea kuvalia vazi hilo,”

Kulthoum anasema ununuaji wa madera na vijora huwa hauna msimu maalumu kwani, watu hupendelea kununua kutokana na mapenzi, wengine hununua kama wakiwa na jambo fulani la muhimu anataka kufanya, kama kwenda kwenye sherehe.

“Watu wengi hununua kwa sababu ya sherehe kama ndoa, kwa ajili ya sikukuu, au ngoma,” alisema

Hata hivyo alieleza kwamba wanawake wengi hupendelea hayo mavazi kwa sababu huwa ni ya bei rahisi ambayo mtu wa hali yoyote huweza kununua.

“Kwa mwezi biashara hutegemea, lakini soko la biashara hii lipo vizuri licha ya kuwapo na changamoto ndogo ndogo.”

Kwa upande wake, Said Almasi mfanyabiashara wa nguo za kike, katika soko la Kariakoo maarufu kama K/koo yeye anasema mavazi aina ya kijora na dera hununuliwa sana kwa sababu ndio mavazi ambayo yanavuma kwa wakati huu.

“Nguo huendana na wakati, kuna kipindi fulani wanawake walikua wanapendelea kuvaa kanga, gauni lakini kwa wakati wa sasa mavazi ya dera na kijora ndio yapo katika soko,” alisema Almasi.

Almasi anasema kabla ya kuanza kuuza vijora pamoja na madera alikua akiuza mavazi mengine ya kike, lakini baada ya kuona mavazi hayo yanapendwa sana akaamua na yeye aanze kuuza aina hizo za nguo.

Comments 0

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles

Latest Post

Latest Tags