Biashara unazoweza kufanya ukiwa kazini

Biashara unazoweza kufanya ukiwa kazini

Katika baadhi ya kampuni si ajabu kukuta mfanyakazi akifanya biashara ndani ya ofisi kama sehemu ya kujiongezea kipato cha ziada.

Kufanya hivyo siyo jambo  baya endapo halitoharibu utendaji kazi wako. Kama wewe ni mmoja wa wanaotamani kujiingizia kipato cha ziada kazini, fanya biashara hizi bila kuingilia majukumu yako mengine.

Vifaa vya ofisini

Katika ofisi yoyote lazima wafanyakazi watumie vifaa kama vile kalamu, Daftari (Notebook) na vingine vingi hivyo kama mfanyakazi unaweza kuchukua fursa hiyo ya kununua vifaa hivyo duka la jumla na kisha kuviuza rejareja kwa wafanyakazi wenzio.

Bidhaa za teknolojia

Bidhaa hizi ni kama vile Chaja, Headphones, Flashi na vingine vingi, kutokana na ukuaji wa teknolojia ufanyaji kazi wa miaka hii unategemeana na vifaa hivi.

 

 

Huduma za kifedha

Huduma za kifedha ni moja ya biashara inayolipa hasa ikipata usimamizi mzuri, unaweza kuifanya popote na muda wowote.

Ukiwa kazini unaweza kufanya huduma ya mitandao ya simu na hata huduma za ki-bank kwa wafanyakazi wenzako, katika sehemu nyingi za kazi watu hukumbwa na uhitaji wa huduma hii lakini huwawia vigumu kuifata sehemu nyingine mbali na ofisini, unapokuwa na biashara hii na hakika hutajutia.

Chakula na vinywaji

Ili kujiongezea kipato chako unaweza kuuza chakula cha mchana au vinywaji kama juice katika ofisi yako kikubwa ni kuwa mbunifu. Katika hili hakikisha kila siku vitu unavyouza vinaladha ya kipekee ambayo mteja wako hawezi kuipata popote hii itakupa wateja wa kudumu.

Andaa vyakula ambavyo havitakuchosha katika uandaaji wake kama vile tambi, chipsi, wali na vinginevyo chakufanya ni kutafuta vijana wanaoweza kupika chakula kizuri wewe jukumu lako likiwa ni kutafuta wateja.

Pia unaweza andaa vitu kama karanga, kashata za ufuta, biskuti na kashata za karanga hivi ni vyakula rahisi vinavyowaliwaza wengi wanapokuwa busy na kazi hivyo kwa wasaka tonge ni biashara nzuri.

Urembo na huduma binafsi

Unaweza uza bidhaa za urembo kama vile Hereni, Mikufu, Saa na kutoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi wenzako kama vile kusuka au kunyoa lakini pia kutengeneza kucha.

Hii unaweza fanya baada ya kazi zako au mwisho wa wiki, hakikisha unafanya kazi yako kwa umahiri ili kujitangaza vizuri na kutengeneza uaminifu machoni pa watu.

Bidhaa za ubunifu

Biashara nyingine ni ubunifu, unaweza kuwa mbunifu wa vitu vya mapambo ya nyumbani na maofisini lakini pia kutengeneza zawadi mbalimbali.

Biashara ya zawadi inaweza kuwa ya msimu lakini unapojitengenezea jina katika ofisi uliyopo wengi watakutegemea kila ifikapo msimu husika.

 

Kikubwa kinachohitajika ni kuwa mbunifu katika uandaaji wako wa zawadi weka kwa namna ambayo kwingine haitapatikana kama yako hii pia ni biashara nzuri

Kikubwa ni kufahamu kuwa watu wengi hufanya biashara na watu wanaowaamini hivyo kuwa mwaminifu, huu ni mtaji namba moja katika biashara yoyote.

Kwa haya machache naimani utakuwa umejifunza na kujua wapi uanzie ili kukidhi mahitaji yako, lakini pia chagua biashara ambayo inakidhi mahitaji ya wafanyakazi wenzako na inauwezo wa kutoa faida nzuri na huduma bora.

 

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post