Biashara 5 bora zakufanya zenye mtaji mdogo

Biashara 5 bora zakufanya zenye mtaji mdogo

Ni kweli ukitaka kuanza biashara lazima ufanye maandalizi, hapa namaanisha unahitaji kuwa na maarifa fulani tofauti kulinganisha na wale uliowakuta ili hata wao pia wajifunze kutoka kwako.

Ikiwezekana na wewe uendelee kujifunza kutoka kwao. Kwenye kipengele hiki tutaenda kuangalia namna ya kufungua biashara ukiwa nyumbani na jinsi ya kutumia kipato kidogo unachokipata ili kufungua biashara nyingine ndogo ndogo ambazo zitaendelea kukuongezea kipato.

Tukianza na maarifa ya kufungua biashara ukiwa nyumbani. Ni vyema ukatambua kuwa na vitendea kazi vichache ili uweze kufungua biashara ukiwa nyumbani.

Vitendea kazi hivyo ni kama jiko la kupikia.  likiwa la kuni sawa au la mkaa. Pia yawezekana ukahitaji mafuta ya kupikia na mihogo au viazi. Maana biashara nnayotaka kuiongelea ya kwanza hapa ni biashara tunayoona kila siku tukipita njiani ambayo ni biashara ya kukaanga mihogo.

Biashara hii ya kukaanga mihogo unaweza ukafanya ukiwa mahali popote iwe ni nyumbani kwako au mahali pengine ambapo unataka. Na maamuzi ya kuchagua eneo yanatokana na wingi wa watu waliopo karibu na wewe.

 

Ukijaribu kuangalia biashara hii kwa ufupi utajikuta unaweza ukaifanya ukiwa nyumbani na pia ni biashara ya mtaji mdogo.

Biashara nyingine ambayo unaweza ukaifanya ukiwa nyumbani ni biashara ya ususi. Kusuka ni biashara mojawapo inayoongeza kipato kwa wanawake wengi.

Ujuzi

Kwanza tukianza kuelezea kwa ufupi kuhusu biashara mbali mbali za kufanya. Ni muhimu tukaelewa kuwa biashara hizi zinaendana na ujuzi.

Ujuzi ndio swala la kwanza kabisa litakalo kupa uhuru Zaidi wa kufanya biashara yeyote. Na biashara ambayo utaifanya haita itaji uwe na kipato kikubwa. Wala eneo maalumu la kuifanyia.

Kwa wale wanaofahamu vijana ambao wanatengeneza baiskeli au pikipiki.  Wale mtaji wao huwa mdogo sana kwa kuanzia. Na kazi zao huwa wanaweza wakazifanya mahali popote. Hii yote ni kutokana na ujuzi walionao.

Tukianza na biashara ya mapishi mbali mbali.

  1. Biashara ya Mapishi

Ukiwa fundi kwenye mapishi ya aina yeyote wateja watakufata ata ukiwa nyumbani. Kikubwa uwe unapika vitu vinavyoeleweka. Kwa wale tunaoona wapishi wanaotembea tu na ndoo na wana pata kipato kizuri.

Ni wazi kuwa wapishi hawa siku wasipopeleka chakula wateja wao huwa wanaanza kuwapigia simu au kuwatafuta ata wakiwa nyumbani ili wapate huduma zao nzuri.

 

Tukiongelea pia mapishi kwenye mikoa yenye baridi. Mapishi haya huusisha mapishi ya chai na mapishi ya vitu vya moto. Mara nyingi wapo watu wanapika tu chai na kuweka chupa nje ya nyumba zao. Na wanapata wateja kwa wingi kutokana na ubora wa chai yao. Hata isipokuwa na vitafunwa.

Na kwa ufupi kabisa mapishi ni sehemu kubwa sana ya biashara zinazowapatia watu kipato. Wakiwa watu wa uwezo wa chini kabisa na wenye uwezo mzuri wa kifedha.

  1. Biashara ya kutengeneza mapambo.

Wale wanaoweza kutengeneza mataji ya kwenye harusi au graduation. Mara nyingi huwa wanapata kipato kizuri sana kwa siku. Na mapambo hayaishii tu kwenye mataji. Bali hata Vidani vya mkononi vya aina mbali mbali.

Na vitu vingine vingi vidogo vidogo. Ambavyo vinavoweza kuwekwa nyumbani na ofisini. Tukiongelea mapambo ni topiki ndefu sana.

Inaweza ikawa wewe ni mchoraji mzuri wa inna. Au kama wewe ni kijana ambae unaweza ukapaka rangi vizuri kucha za wadada.Inawezekana pia wewe ni mbunifu uliekuja nap ambo lako jipya la kuvaa au kuweka nyumbani kwa mtu.

Lakini ukishajua vizuri wateja wako. Na ukaanza kuwatengenezea kutokana na mahitaji yao. Vitu kama maboksi mazuri ya kuwekea zawadi.

Au vitu vingine ambavyo utaviongezea akili yako ili viwe vya urahisi kutumia. Lakini vinakusudi la kuwa kama pambo. Ukweli ni kwamba utapata watu wa kotosha ambao watakutafuta hata ukiwa nyumbani.

 

  1. Biashara ya uandishi

Ukiweza kuwa mwandishi mzuri ambae anaandika stori zake kwa umakini. Au anaandikia watu na anaweza akachapisha. Utajikuta unaandika kwanzia vitabu vya shule za msingi ambavyo vinapendwa sana.

Na unavichapisha na vinauza vizuri tu. Biashara hii haiitaji mtaji mkubwa bali inahitaji wewe kuanza kupata wateja wa kwanza.Na hao wateja utakao anza nao ndio watakuletea wateja wengine. Na ukishaanza kujulikana utaweza kufanya biashara kama hii ata ukiwa nyumbani.

Kwa yule anaetaka kuanza biashara ya uandishi.  Unaweza ukaanza kwa kununua tu flashi.

Ambayo ina gb 1 au 2 kwa shilingi elfu 7 au 8. Na kwa kuanza unaweza kuwa unaenda vyumba vya kukodisha huduma za computer (Tanakilishi) ili uanze kutengeneza maandishi ambayo unataka yawafikie watu wengi.

Yawezekana ukawa umeshaa andaa kitu unachotaka kukiandika ili usipoteze mda sana. Ukishamaliza kukiandaa ndio unaenda kukiandika kwa kupitia computer. Sikuhizi huduma hii ipo ata kwenye simu janja kama unataka tu kuandika story za kuwauzia Watoto.

Swala la kuchapisha na kuweka na jalada zuri nje, ni swala la wachapishaji. Kutokana na mahali ulipo fanya jitihada za kuwajua wachapishaji waliopo kwaribu na wewe na uanze kazi yako ya uandishi.

 

  1. Biashara ya vitu vya kupaki

Vitu vya kupaki kama, ice cream, biskuti, maji, soda, juisi, pipi, mikate. Na vinginevyo ni biashara inayowaongezea sana vijana kipato kizuri cha kujikimu.

Kwa wale walio karibu na viwanda vya mikate, Unaweza ukachukua mikate yako ya kutosha na ukapelekea watu wa maduka au ukapeleka kuuza mwenyewe.

Unaweza ukajiuliza je biashara hii inaendana na biashara ya kufanya ukiwa nyumbani?  Na jibu ni ndio, pale tu utakapo kuwa kwenye eneo lenye watu wengi.

Au kama unaweza ukawa na kijana mwaminifu wa kumwagiza kufanya biashara hio kila siku akuletee mahesabu. Njia zipo nyingi sana za kufanya biashara ile ile unayoiona inafanyika kila siku.

5. Biashara ya miche ya miti na mbegu

Ukiangalia biashara hii unaweza ukasema ni kitu kigumu sana. Lakini ukweli ni kwamba kila siku tunakutana na miti njiani na pia tunakutana na mimea mbali mbali.

Lakini shida ni kwamba hatufanyi uchunguzi wa kutosha wa jinsi ya kuotesha mimea hio. Tukianza na jinsi ya kujua namna ya kuotesha ni elimu inayotolewa bure kabisa mtandaoni. 

Ikiwemo kwenye mitandao ya kijamii na mitandao mingine yote kama youtube. Sa nyingine kwa wale ambao wanaona kujifunza wenyewe ni tabu. Kosa ni kwamba hawajawahi ata kwenda kuwauliza wale waonao uza miche. Ukaamua kukaa nao hadi ukaanza kujua jinsi ya kuiotesha. Kuna miti mingine ipo imeota ata nyumbani kwako.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags