Bi Ubwa wa Zahanati ya Kijiji afariki dunia

Bi Ubwa wa Zahanati ya Kijiji afariki dunia

Aliyekuwa mwigizaji wa tamthilia ya Zahanati ya Kijiji,  Bi Ubwa amefariki dunia leo Jumamosi Aprili 20, 2024, mtayarishaji wa tamthilia hiyo  Abdully Usanga amethibitisha taarifa hiyo ambayo ameipokea kutoka kwa mtoto wa marehemu.

 

Hata hivyo mpaka sasa bado haijafahamika chanzo cha kifo chake.

@mwananchiscoop imezungumza na mmoja kati ya waigizaji wa Zahanati ya Kijiji  John Elisha ameeleza kuwa  amepokea taarifa hizo masikitiko makubwa.

“Nimepokea ghafla, kazi ya Mungu haina makosa na alikuwa mama yetu mcheshi na mwenye upendo” amesema John.

Bi Ubwa kutokana na umahiri wake katika ugizaji aliwahi kuonekana katika thamthilia mbalimbali zikiwemo ‘The Spirit’, Zahanati ya Kijiji, Simu, Penzini, Nuru.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags