Beyonce, Jay Z Waondolewa Kesi Ya Diddy

Beyonce, Jay Z Waondolewa Kesi Ya Diddy

Majina ya mwanamuziki Jay Z na mke wake Beyonce yameondolewa katika kesi ya Diddy ambayo imefunguliwa mapema mwezi huu, kesi ambayo inahusiana na usafirishaji haramu wa binadamu.

Aprili 1, 2025 mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Manzaro Joseph aliwasilisha kesi mahakamani akidai kudhalilishwa mbele ya watu mashughuli akiwemo Beyoncé, JAY-Z, LeBron James, na Gloria Estefan wakati wa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mtoto wa Diddy, Christian “King” Combs, iliyofanyika Star Island mwezi Aprili 2015.

Aidha aliweka wazi kuwa licha ya kudhalilishwa mbele za watu wasanii hao wakubwa walibaki kuuliza na kucheka kinachoendelea bila ya kufanya chochote kuzuia udhalilishaji huo.

Hata hivyo wakili wa JAY-Z, Alex Spiro, aliiambia TMZ, kuwa Jay hakuwa Florida wakati huo alikuwa akishiriki katika shughuli nyingine za wazi ambazo zinaweza kupatikana kwenye baadhi ya kumbukumbu za video zake huku akiweka wazi kuwa madai hayo ni yauongo.

Baada ya wakili kuthibitisha hilo mshitaki Manzaro alibadilisha rasmi mashitaka yake akiondoa majina ya Beyoncé na JAY-Z katika kesi hiyo huku akiendelea kuwashitaki Diddy, Emilio Estefan, Adria English, pamoja na anayedaiwa kuwa msafirishaji wa dawa za kulevya wa Combs, Brendan Paul, pamoja na watu wengine kadhaa wasiojulikana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags