Beyonce Apigwa Marufuku Na Mmiliki Wa Sphere

Beyonce Apigwa Marufuku Na Mmiliki Wa Sphere

Mmiliki wa ukumbi wa Sphere uliopo Las Vegas amemtumia Beyoncé barua ya kuzuia na kusitisha (cease and desist) kipande cha video kilichorekodiwa na mashabiki katika tamasha lake, kipande ambacho kinaeleza kuwa Beyonce ni mkubwa kuliko ukumbi huo.

“Beyoncé akiwa mkubwa sana kwa viwango vikubwa kuliko ukumbi wa Sphere anainama, anauchukua ukumbi huo, na kusimama juu yake kwa namna ya kutisha,” imesikika sauti katika video hiyo

Aidha kutokana na video hiyo Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Madison Square Garden Entertainment Group, amemtaka Beyoncé aondoe kipande hicho kifupi cha video kutoka kwenye tamasha lake la saa tatu, ambalo alilitumbuiza kwa mara ya pili ‘SoFi Stadium’ huko Los Angeles siku ya Alhamisi (Mei 1).

Barua hiyo iliyoandikwa na wakili Kathleen McCarthy, anaituhumu Parkwood kwa kutumia picha za ukumbi wa Sphere bila kupata kibali rasmi. Pia, anadai kuwa hatua hiyo imewachanganya na kuwapotosha mashabiki wa Beyoncé kwa kuashiria uhusiano au ushirikiano ambao haupo kati ya msanii huyo na ukumbi huo.

Aidha Sphere wameipiga marufuku timu ya Beyonce kurekodi ukumbi wao bila idhini na endapo video hizo zisipofutwa basi watamfungulia kesi Beyonce.

Ikumbukwe kwamba siku ya Alhamisi, Beyoncé alikuwa akitumbuiza katika uwanja wa ‘SoFi Stadium’, ambao uko karibu na ukumbi wa Sphere. Timu yake ya utayarishaji ilichukua video inayoonesha mandhari ya ukumbi wa Sphere, jambo ambalo limesababisha tetesi kubwa kuwa huenda Beyoncé anamakubaliano na ukumbi huo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags