Best Naso ataja chanzo cha kuzushiwa kifo

Best Naso ataja chanzo cha kuzushiwa kifo

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Best Naso amefunguka na kueleza chanzo cha yeye kuzushiwa kifo hivi kariubuni.

Msanii huyo alisema kwamba taarifa za kuzushiwa kifo zilianzia kwenye mtandao mmoja kutoka nchini Kenya ambapo uliposti kuwa amejinyonga.

Hata hivyo inaelezwa kuwa taarifa hizo za kifo zilisababisha bibi yake kuzimia mara tatu kijijini na kuleta taharuki kubwa kwenye familia yake.

“Maisha ya sasa hivi yamekuwa ni biashara, kwa sababu hao watu waliofikiria kunizushia mimi kifo walijua watapata views kwenye akaunti zao na kupata kipato.

“Ila mimi kama msanii ninaona ni kitu cha kawaida, niwaambie tu Naso yupo na ndio maana ameachia albamu yake ambayo ina nyimbo 32 lengo ni kuwaonesha nipo na nina afya njeama,” alisema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags