Benzio: R.Kelly anastahili nafasi ya pili

Benzio: R.Kelly anastahili nafasi ya pili

Mmiliki wa vyombo vya habari na ‘rapa’ kutoka nchini Marekani Raymond Scott, maarufu ‘Benzino’ amemkingia kifua mkali wa R&B, R. Kelly akitaka msanii huyo aachiwe huru na apewe nafasi ya pili ya kujirekebisha.

Benzino wakati akiwa kwenye mahojiano na podcast ya ‘We In Miami’ ameeleza kuwa miaka aliyohukumiwa Kelly ni mingi sana hivyo basi ameiomba mahakama kumuachia huru kwani katika maisha kila binadamu anahitaji nafasi ya pili ya kujirekebisha huku akienda mbali zaidi akidai kuwa baadhi ya kesi zinazomkabili Kelly amebambikiziwa.

Septemba 2021, Kelly alikutwa na hatia ya makosa tisa yakiwemo ya ulaghai na ulanguzi wa ngono dhidi ya watoto chini ya umri wa miaka 15 ambapo alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela Juni 2022.

Hata hivyo wiki kadhaa zilizopita Waendesha mashitaka walimuomba hakimu amuongezee kifungo cha miaka 25 mwanamuziki huyo atakapo maliza kifungo cha miaka 30 lakini jaji wa Mahakama ya kati jijini New York, Harry Leinenweber alikataa na kuamuru Kelly atumikie kifungo cha miaka 20 na cha awali kwa wakati mmoja.

Robert Sylvester (57) maarufu ‘R. Kelly’ alizaliwa Januari 8, 1967 Chicago nchini Marekani na alikuwa akitamba na ngoma zake kama ‘I Believe I Can Fly’, ‘Apologies of a Thug’, ‘Step In the Name of Love’,  ‘I’m Your Angle’, ‘Same Girl’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags