Benzema anavyopiga mshahara kidogo, pesa nyingi

Benzema anavyopiga mshahara kidogo, pesa nyingi

Its onether weekend!! Mtu wangu mambo vip, kama kawaida katika michezo hatuna muda wa kucheleweshe mapema tunakusogezea yalio jiri katika burudani na michezo.

Leo katika Burudani/michezo nimekusogezea mwanasoka maarufu duniani kwa kuwa na umahiri katika ulimwengu wa soka na kupata mafanikio kadha wa kadha si mwengine ni Benzema.

Karim Benzema kijana mwenye asili ya Algeria na kubarikiwa na uraia pacha Ufaransa na Algeria kwenye klabu yake ya Real Madrid wame mteuwaa kuwa kapteini watimu hiyo.

Benzema mpaka sasa akiwa na miaka 34, bado anaonekana kuwa msaada kwenye timu na mashabiki wengi wangetamani kumuona akiendelea kusalia kwenye viunga hivyo kwa muda mrefu kutokana na mchango wake ambao amewezesha klabu yake ya Real Madrid kushinda taji la Ligi ya Mabingwa.

Licha ya mchango wake mkubwa kwa timu hiyo jamaa sio mchezaji anayelipwa pesa nyingi, pengine hiyo ni kutokana na umri wake na mkataba mpya aliosaini mwaka jana.

Lakini hiyo haionekani kumshtua sana kwani jamaa ana utajiri wa kutosha na bado anaendelea kupiga pesa kutokana na vyanzo mbali mbali.

 

JINSI ANAVYOVUNA PESA

Anapokea mshahara wa Pauni 170,000 kwa wiki ambao ulipungua kutoka Pauni 290,000 aliokuwa anaupata hapo awali kabla ya kusaini mkataba wa mpya mwaka jana.

Lakini bado kiasi hicho cha pesa kinamfanya kuwa mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa vizuri kwenye viunga hivyo vya Bernabeu.

Mbali ya mshahara anapata pesa kupitia madili ya nje ya uwanja kama ilivyo kwa mastaa wengine ambapo yeye analipwa na kampuni ya Adidas, Hyundai,  EA Sports na Bwin.

Pia ameingia kwenye mikataba ya ubalozi na kampuni za nchini kwao ambazo ni LCL (Le Credit Lyonnais) na SFR (Societe francaise du radiotelephone).

Kwenye sekta mwamba anapiga pesa nyingi nje ya uwanja anakadiriwa kupata kiasi kisichopungua Pauni 20 miloni kwa mwaka mmoja kutokana na mjumuisho wa  madili yote hayo kiujumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 70 milioni.

MSAADA KWA JAMII

Benzema kwa sasa anafanya kazi na taasisi ya Charity Stars ambayo ufanyaji kazi wake huwa hivi, mchezaji huhitajika kutoa jezi au viatu vyake alivyochezea mechi na kuweka saini yake kisha vinawekwa sokoni na taasisi hiyo kisha baada ya hapo zile pesa zinazopatikana baada ya hicho kitu kuuzwa huwa zinatumika kusaidia watu wenye uhitaji waliokumbwa na matatizo mbali mbali.

Pia licha ya utukutu wake awapo nje ya uwanja, mara kadhaa amekuwa akiisaidia jamii ya watu wa karibu wanaomzunguka huko nchini kwao Ufaransa.

NYUMBA ANAZO MILIKI

Mbali yakuwa na nyumba nchini Ufaransa ambayo taarifa zake bado hazijajulikana, jamaa pia anamiliki bonge la jengo huko nchini Hispania ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya Dola 2.7 milioni na ndani ya mjengo huo mbali ya mandhari nzuri pia kuna bwawa la kuogelea na eneo kubwa ambalo humuwezesha kufanya mazoezi anapokuwa nyumbani.

 

MAGARI ANAYO MILIKI

Benzema bwana tuseme tu sijui anapenda zaidi magari kuliko starehe nyingine kwani ametumia kiasi kikubwa cha pesa kwenye kununua gari nyingi zenye thamani kubwa.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun, inaripotiwa kuwa jumla ya magari yake yote ni Pauni 6 milioni ambayo ni zaidi ya bilioni 12 za kibongo. Hizi ni miongoni mwa gari zake ambazo nyingine zilitengenezwa kwa oda maalumu moja kwa  moja kutoka kiwandani.

Bugatti Chiron-Pauni 2.5 milioni

Ferrari 458 Spide-Pauni 1.5 milioni

Mercedes Benz-SLR- Pauni 750,000

Audi RS6- Pauni 90,000

Ferrari 458 Spider-Pauni 200,000

RS6 Avant C7 -Pauni 90,000

Bugatti SUV-Pauni 40,000

Rolls Royce Pauni- 250,000

Lamborghini Gallardo-Dola 214,001

Mercedes-AMG Classe G63 -Pauni 140,000

450 Bugatti Veyron-Pauni 1.5 milioni

Sambamba na hayo Benzema Yupo kwenye ndoa na mrembo Cora Gauthier ambaye walifikia uamuzi wa kuoana Desemba, 2016 ikiwa ni mwaka mmoja tangu walipoanza kuwa kwenye uhusiano.

Baada ya ndoa Cora Gauthier alipata ujauzito na kuzaa mtoto wa kiume ambaye alipwa jina la Ibrahima.

Wakati wawili hao wanafunga ndoa tayari Benzema alishapata mtoto wa kike kutoka kwa mwanamke mwingine, lakini kwa sasa mtoto huyo anakaa naye mwenyewe na mkewe Gauthier.

Kutokana na majukumu ya familia Benzema sio mtu wa kujirusha sana na hata akionekana kwenye pande hizo huwa sambamba na mkewe na watoto wao.

Nyie nyiee!!! Katika wanasoka wanao upiga mwingi kifedha huwezi kumuacha huyu mwamba mimi narudia tena kuwaambia fursa ni muhimu sana, ana jitihada mno kuhakikisha familia yake inaishi maisha bora sometime hakuna uchawi kwenye mafanikio ni kupambana tuu.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags