Bayern yamuandalia Kane mjengo wa kifahari

Bayern yamuandalia Kane mjengo wa kifahari

Wakati ‘dili’ la kwenda Bayern Munich likiwa halieleweki kuna taarifa zinadaiwa kuwa kuna uwezekano mchezaji Harry Kane akaendelea kusalia Tottenham, tetesi za ndani zinadai Bayern Munich imemuandalia mjengo wa kifahari ‘staa’ huyo ikiwa ni moja ya maandalizi ya kukamilisha uhamisho wake.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Mirror, Bayern imemuandalia Kane mjengo wa kifahari uliopo nje ya kidogo ya Jiji la Munich ambako wanakaa ‘mamilionea,’ mbali na hilo inaelezwa kuwa team hiyo imemuandalia hadi sehemu ya kukaa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo katika dimba la Allianz Arena.

Hata hivyo mbali ya maandalizi yote hayo, taarifa zilizopo hivi sasa ni kwamba kuna uwezekano wa  Kane akaendelea kusalia kwenye viunga vya Spurs kwa msimu ujao kwani ‘ofa’ ya mwisho ya Munich haikutolewa majibu na mwenyekiti wa ‘timu’ hiyo Daniel Levy na mwisho wa kufanya hivyo ilikuwa ni Ijumaa ya ‘wiki’ iliyopita.

Spurs inadaiwa kuhitaji walau Pauni 100 milioni ili kumuuza Kane ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags