BATA BATANI: Kimondo cha Mbozi

BATA BATANI: Kimondo cha Mbozi

Alright my traveling and adventure peeps. Ni wiki nyingine tena tunakutana hapa katika segment ya BATA BATANI. Basi bwana, wiki hii nipo na Kimondo cha Mbozi, Songwe.

Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kilianguka kutoka anga-nje karibu na mji wa Vwawa.  Kinakadiriwa kuwa na uzito wa takriban tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenje.

Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma  ni 90.45%, nikeli   8,69%, Sulfur 0,01% na fosfori 0,11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana.

Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko:  kwa hiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko.

Goodluck exploring this meteorite!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags