Barnaba atoa sababu Harmonize kutokuwepo kwenye albam yake

Barnaba atoa sababu Harmonize kutokuwepo kwenye albam yake

Na Habiba Mohammed

Niajeeee niajeeeeee! Kama kawa kama dawa yaani tunahakikisha kila chochoro tunakuletea stori za motooooo. Ebwaaaaana eeenh kwenye mitandao yote ya kijamii lugha ni moja tuu yaani mikwaju mikarii ya msanii  mkongwe wa bongo fleva Barnaba classic aka Mopao,  na kubwa Zaidi ni kuhusu Album yake ya love sounds different (LSD).

Barnaba alifanya uzinduzi wa Album yake tarehe agosti ,17 kupitia Album yake yenye nyimbo 19 akiwa ameshirikisha wasanii mbalimbali ikiwemo Diamond plantinum ambaye pia ni Executive producer wa Album hiyo,vilevile Marioo,Lord music,Kusah,Saraphina,Alikiba pamoja na komando jide Lady jaydee .

Kama ilivyokawaida walimwengu hatuishiwi jambo ,kunako kurasa ya Instagram ya Barnaba classic comment zilikuwa nyingi za kumpongeza lakini pia na mswali kutoka kwa mashabiki zake ,moja ya swali linalozungumzwa sana ni Harmonize kutokuwepo kwenye Album hiyo, Barnaba katika mahojiano aliyofanya na moja ya chombo maarufu cha habari alijibu swali hilo kwa kusema kuwa

“Love Sounds Different Album ambayo nimejaribu kuwaleta pamoja wasanii wa level tofauti tofauti za mziki wa bongo fleva thus why nimeshirikisha wasanii wapya,wakongwe na wasanii wakubwa,kuhusu swala la Harmonize kutokuwepo kwenye Album yangu haimaanishi tunaugomvi ,Hapana ila kipindi na muhitaji alikuwa na majukumu mengine na ni busara kuheshimu taratibu za mtu na mimi kuendelea kufanya taratibu zingine kukamilisha Album yangu”amesema

Aya sasa walimwengu Mopao kayasema ya moyoni hakuna ugomvi wala kuvimbiana ni swala la menejimenti,tutegemee mazuri kutoka kwa Barnaba na mmakonde Harmonize siku zijazo.

Byeeee byeee!!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags