Bango la picha ya Ronaldo laondolewa uwanjani Old Trafford

Bango la picha ya Ronaldo laondolewa uwanjani Old Trafford

Saa chache kabla ya mahojiano ya nyota wa Manchester United Cristiano Ronaldo na Piers Morgan kupeperushwa hewani, klabu hiyo imeondoa bango kubwa lenye picha ya ukutani ya mchezaji huyo iliyokuwa nje ya uwanja wa Old Trafford.

Sehemu za mahojiano hayo tayari zilikuwa zimechapishwa siku ya Jumapili, ikiwemo vipande vilivyomuonyesha Ronaldo akisema anahisi kusalitiwa na Manchester United na kuwa, hamuheshimu kocha Eric ten Hag.

Ronaldo alitumia mahojiano hayo ya sehemu ya kwanza ya dakika 90 kuwakashifu wamilki wa Manchester United-familia ya Glazers, kocha wake na baadhi ya wachezaji wenzake.

 Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos amesema mahojiano hayo hayajatatiza matayarisho ya timu hiyo kuelekea mechi ya kirafiki dhidi ya Nigeria leo Alhamisi, mechi ya mwisho ya timu hiyo kabla ya kwenda Qatar kwa kombe la dunia.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post